Mfuko wa Mawasiliano (USCAF) umekabidhi Kompyuta 5 na Printer 1 zenye thamani ya shilingi 11,000,000 kwa Shule ya Sekondari Mtumba, hafla iliyohudhuriwa na Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini Mhe. Anthony Peter Mavunde, Diwani wa Kata ya Mtumba Mhe. Edward Maboje, wazazi na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mtumba siku ya Ijumaa ya tarehe 13 Machi, 2020
Pamoja na makabidhiano hayo Mbunge Mavunde pia alikagua ujenzi wa jengo la Maabara ambalo aliweka jiwe la msingi mwaka 2016.
Katika kuunga mkono jitahada za Uongozi wa Shule na nguvu za wananchi Mbunge huyo amechangia mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wanafunzi, kuweka umeme nyumba za Walimu na vifaa vya michezo.
Naye Diwani wa Kata ya Mtumba, Mhe. Edward Maboje amemshukuru Mbunge Mavunde kwa namna ambavyo amesaidia kutatua changamoto za sekta ya Elimu katika kata hiyo na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano katika kuhudumia wananchi.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde akiwahutubia wazazi na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mtumba leo wakati wa Hafla ya kukabidhi Kompyuta 5 Printer 1 zenye thamani ya Tsh 11,000,000 zilizofadhiliwa na Mfuko wa Mawasiliano. (USCAF).
Diwani wa Kata ya Mtumba, Mhe. Edward Maboje ameushukuru Mfuko wa Mawasiliano (USCAF) na Mbunge Mavunde kwa namna ambavyo amesaidia kutatua changamoto za sekta ya Elimu katika kata hiyo na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwao.
Kwa furaha kikundi cha utamaduni kutoka Kata ya Mtumba wakitumbuiza wakati wa hafla ya makabidhiano ya kompyuta na printer kwa shule ya sekondari Mtumba.
Vifaa vya TEHAMA zikiwemo Kompyuta na 'Printer' vilivyokabidhiwa kwa Shule ya Sekondari ya Mtumba.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini Mhe. Peter Mavunde akikagua ujenzi wa Maabara ya sayansi, jengo ambalo Mhe. Mavunde aliweka jiwe la msingi mwaka 2016.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mtumba siku ya kukabidhiwa kompyuta na printer.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.