• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Ushirikiano kati ya tanzania na canada waipaisha sekta ya afya

Imewekwa tarehe: July 21st, 2025

Na WAF - Dsm

Mahusiano mazuri ya kidiplomasia na ushirikiano wa maendeleo baina ya Tanzania na Canada umeendelea kuipaisha Sekta ya Afya nchini hivyo kuboresha zaidi ubora wa huduma za afya ngazi ya msingi.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhgagama leo Julai 20, 2025 mara baada ya kumpokea Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Canada Mhe. Randeep Sarai pamoja na ujumbe aliyoambatana nao kutoka nchini Canada waliowasili kwa ziara ya kikazi ya siku tano (5) nchini.

“Tunaishukuru na kuipongeza Serikali ya Canada kwa kuendelea kuwa mshirika wa maendeleo ya Sekta ya Afya nchini Tanzania, kwa mchango wanaoutoa kwenye mfuko wa pamoja wa afya (Health Basket Fund) ambao unasaidia katika uboreshaji wa huduma za afya ngazi ya msingi kupitia mfumo wa ufadhili wa moja kwa moja katika vituo vya Afya awamu ya kwanza (2022–2027),” amesema Waziri Mhagama.

Waziri Mhagama amebainisha kuwa Tanzania imekuwa ikishirikiana na Serikali ya Canada katika kuboresha huduma za afya ya uzazi, haki za vijana balehe pamoja na kuimarisha huduma za uuguzi wakati wa kujifungua ambazo zinalenga kupunguza vifo vya mama na watoto wachanga kwa kuongeza upatikanaji wa wakunga wenye ujuzi.

“Ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Canada katika sekta ya afya umeleta mafanikio mengi ikiwemo kupungua kwa vifo vya watoto chini ya miaka mitano kutoka asilimia 67 mwaka 2015 hadi asilimia 43 mwaka 2022 kwa kila vizazi hai 1,000, kupungua kwa vifo vya akina mama wakati wa kujifungua kutoka 556 hadi 104 kwa kila vizazi hai 100,000,” amefafanua Waziri Mhagama.

Waziri Mhagama hakusita kuelezea changamoto ya kasi ndogo ya kupungua kwa vifo vya watoto wachanga, kutoka vifo 25 kwa kila vizazi hai 1,000 mwaka 2015 hadi vifo 24 kwa kila vizazi hai 1,000 mwaka 2022 na kutumia fursa hiyo kuiomba Serikali ya Canada kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kutekeleza afua za afya zinazolenga kutatua changamoto hiyo.

Kwa upande wake, Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Canada Mhe. Randeep Sarai ameshukuru kwa mapokezi mazuri nchini Tanzania na ameahidi nchi hiyo kuendelea kutoa ushirikiano hasa katika Sekta ya Afya.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Shekimweri: Maafisa tarafa na Watendaji wa kata zingatieni Maadili na Uwajibikaji

    July 23, 2025
  • Serikali yatoa bilioni 298 kugharamia matibabu ya Kifua kikuu, Ukimwi na Malaria nchini

    July 22, 2025
  • Ushirikiano kati ya tanzania na canada waipaisha sekta ya afya

    July 21, 2025
  • Vifaa vya kupima maji vitumike mara baada ya mafunzo

    July 20, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.