USAID Kizazi Hodari Kanda ya Kusini ni mradi unaofadhiliwa na watu wa Marekani kupitia shirika ya misaada la USAID. Mradi huu unatekelezwa na shirika la Deloitte Consulting kwa kushirikiana na taasisi za kiraia (CSOs) na wadau wengine muhimu katika mikoa kumi na moja nchini Tanzania. Ushirikiano huuunalenga kuimarisha uhusiano kati ya vituo vya afya na jamii, kujenga uwezo, na kutoa huduma bora kwa walengwa.
Mradi unalenga kuboresha upatikanaji wa huduma za afya, ustawi, na ulinzi kwa Watoto Yatima na Vijana wanaoishi katika mazingira hatarishi (OVC) katika jamii zenye idadi kubwa ya maambukizi ya VVU ndani ya Kanda ya Kusini ya Tanzania. Mradi unalenga kuchangia Malengo ya 95-95-95: kuhakikisha kwamba ifikapo mwaka 2030, asilimia 95% ya Watu Wanaoishi na VVU (PLHIV) wanajua hali yao, asilimia 95% ya PLHIV wanaojua hali yao wanapata matibabu, na asilimia 95% ya PLHIV wanaopata matibabu wanapata kufubaza VVU.
Ili kuhakikisha uendelevu na kuendana na vipaumbele vya kitaifa, Mradi wa USAID Kizazi Hodari Kanda ya Kusini unafanya kazi kwa karibu na wizara tatu: Wizara ya Afya, TAMISEMI, na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, pamoja na Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS). Ushirikiano huu ni muhimu katika kuongeza uwezo wa kusimamia, kuboresha, na kuendeleza upatikanaji wa huduma na mifumo ya kusaidia OVC, na kuendeleza mchango wa mradi katika kudhibiti janga la UKIMWI.
Mnamo Tarehe 21 Juni 2024, wafanyakazi wa mradi wa USAID Kizazi Hodari Kanda ya Kusini walikutana na wadau muhimu wa Serikali mjini Morogoro kujadili mapendekezo ya utekelezaji wa mradi kwa mwaka wa fedha (FY25) utakaoanza Oktoba mosi 2024 na kukamilika Septenmba 2025. Kikao hiki cha siku mbili kilijumuisha mawasilisho ya mpango kazi uliopendekezwa, ambapo wawakilishi wa serikali walitoa michango na mapendekezo muhimu ili kuhakikisha mipango ya mradi inaendana na vipaumbele vya Serikali na upatikanaji wa huduma bora kwa walengwa.
Baada ya mawasilisho, mjadala mkubwa ulijikita katika maeneno tofauti, ikiwa ni pamoja na uendelevu wa mradi, kujengeaa uwezo wa wahudumu wa afya ngazi ya jamii, kushirikisha wadau mbalimbali katika ngazi tofauti, kuboresha mfumo wa rufaa kati ya vituo vya kutolea huduma za afya na watoa huduma ngazi ya jamii na kuimarisha mifumo ya serikali. Wawakilishi wa serikali walitoa ushauri muhimu juu ya kuboresha ushirikiano na kuhakikisha uendelevu baada ya mradi kuisha.
Washiriki wa kikao hicho walitembelea maeneo mbalimbali ya mradi, ikiwemo vituo vya afya, kaya, na vikundi vya kuimarisha uchumi. Madhumuni ya ziara hizi ilikuwa ni kuongeza ufahamu zaidi juu ya malengo mahususi ya mradi na namna unavyoboresha maisha ya walengwa.
Tunatoa shukrani zetu za dhati kwa wizara kwa ushirikiano wao endelevu. Ushirikiano huu ni muhimu katika nia ya kufikia malengo ya mradi ya kulinda na kuboresha maisha ya Watoto Yatima na Vijana wanaoishi katika mazingira hatarishi katika Kanda ya Kusini ya Tanzania
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.