WANANCHI wametakiwa kujiepusha na ununuzi wa mashamba bila kuzingatia taratibu za Mipango Miji na kupatiwa hati ya umiliki na muuzaji ndani ya Halmashauri ya jiji la Dodoma ili kuepuka hasara .
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Godwin Kunambi alipokuwa akiongea na wananchi wa Kata ya Nzuguni jana kufuatia kukamilika kwa zoezi la upimaji shirikishi katika eneo la Nzuguni ‘A’.
Kunambi alisema “Halmashauri ya Jiji la Dodoma sasa ni Makao Makuu ya Nchi hivyo napenda kuwahakikishia kuwa sheria za ardhi zinasimamiwa barabara…Mtanzania yeyote asinunue shamba bila hati kwani ardhi au shamba au kiwanja hakikisha unapata hati ya umiliki” alisisitiza.
Alisema kuwa Halmashauri ya Jiji ipo katika hatua za mwisho kukamilisha mpango kabambe, hivyo, eneo lote la Halmashauri hiyo litakuwa limepangiwa matumizi ya ardhi.
“Hivyo, unaweza kununua eneo, kumbe eneo hilo limepangwa kupandwa msitu, au barabara hakutakiwa na fidia…tunahitaji Halmashauri ya Jiji la Dodoma iwe na hadhi ya Makao Makuu ya Nchi” alisema Kunambi.
Akiongelea viwanja vitakavyogawiwa kwa wananchi, Mkurugenzi huyo aliwashauri kufuata taratibu za ujenzi.
“Ndugu zangu, ukipata kiwanja, ukishakilipia, andaa ramani vizuri kisha nenda Ofisi za Halmashauri kuomba kibali cha ujenzi ili uanze kujenga” alisema Kunambi.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.