Mtaa wa Nduka ambao upo katika Kata ya Chamwino, Halmashauri ya Jiji la Dodoma, umeendelea kutekeleza Mkataba wa Lishe kwa kufanya maadhimisho ya siku ya Afya na Lishe ya Kijiji/Mtaa (SALIKI),
Lengo la kufanya Maadhumisho hayo katika ngazi ya Mtaa ni kutoa Elimu ya kuzingatia lishe Bora ikiwa ni kupunguza/kumaliza athari zinazotokana na Lishe Duni hasa Kwa Wajawazito na watoto chini ya umri wa Miaka Mitano pamoja na Jamii nzima.
Maadhimisho haya yameshuhudiwa na Viongozi wa Mtaa wakiongozwa na Mwenyekiti wa Mtaa wa Sokoine Ndugu *Mohamed Pampai*, Afisa Mtendaji Bi. *Kulthum Ally* , wajumbe wa serikali za Mtaa pamoja na Mabalozi huku Mgeni rasmi akiwa Afisa Lishe kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma Bi.*Frida Mollel*
Mtaa wa Nduka umefanikisha Maadhimisho haya kwa kushirikiana na Wataalamu kitoka *Zahanati ya Chamwino*
Huduma zilizotolewa ni pamoja na elimu ya Afya na lishe, upimaji wa macho, maonesho ya makundi matano ya vyakula na upikaji wake, upimaji wa afya ukihusisha kupima BP, HIV, Malaria, uzito na urefu (BMI) pamoja na kutoa vyeti kwa watoto wadogo, Matone ya vitamin "A" na dawa za miyoo kwa watoto chini ya Umri wa miaka 5.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.