Serikali ya awamu ya sita (6) inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeanza rasmi utekelezaji wa Mpango Jumuishi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii Mkoani Geita.
Akifungua Kikao cha Uraghibishaji wa Mpango huo kwa Viongozi Waandamizi wa Mkoa, Wilaya, na Halmashauri, Mhe. Said Nkumba Mkuu wa Wilaya ya Chato kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Geita amesema Mpango huo una mchango mkubwa.
“Mpango huu sasa utasaidia kuimarisha jitihada za kuinua hali ya utekelezaji wa huduma za Afya ngazi ya jamii ili kufikia Afya kwa wote”.amesema.
Ameendelea kufafanua kuwa kupitia Mpango huu, Mkoa utakuwa na matokeo mazuri zaidi katika wigo mpana wa Afya kwa ujumla ikilinganishwa na hapo awali .
“Tulijikita katika maeneo kadha wa kadha hususan katika eneo la utoaji wa elimu na hamasa kwa jamii kupitia Wahudumu 1134 waliokuwepo awali,hivyo kupitia Mpango huu utakuwa na matokeo mazuri”amesema.
Nae Katibu Tawala wa Mkoa (Ndg. Mohamed Gombati) amezitaka ngazi zote za kiutendaji kuepuka njama, dhuluma, rushwa au udanganyifu wowote unaoweza kuharibu ufanisi na ubora wa utekelezaji wa Mpango huu “leo mtaona tumejumuisha Viongozi wenzetu wa Usalama na TAKUKURU ngazi ya Mkoa, hivyo niwaombe pia mkafanye hivyo hivyo katika maeneo yenu ili tufanikiwe kwa pamoja”amesema.
Aidha, Katibu Tawala huyo amezitaka Halmashauri kukamilisha kwa haraka zoezi la kuwatambua Wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii (mapping CHW) waliopo ili kutokwamisha jitihada hizi nzuri za Serikali.
Akitoa salamu za ukaribisho na utambulisho, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita Dkt. Omari Sukari amewaomba Viongozi watendaji wa Idara ya Afya ndani na Mkoa na Halmashauri zote kuzingatia mwongozo wa programu na maelekezo ya Viongozi na kushiriki vema ili kusaidia utekelezaji wa Mpango huu.
Kwa upande wao Wawakilishi kutoka Wizara ya Afya, na Ofisi ya Rais TAMISEMI(Bw. Simon Nzilibili na Mathew Mganga) waliwezesha mawasilisho mawili yaliyolenga kuongeza uelewa, hamasa na taratibu za kufuata katika kuchagua na kutekeleza Mpango huo jumuishi na hatimaye kuimarisha huduma za afya
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.