MKUU wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge ameipongeza Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa hatua yake ya kununua magari mapya kwa ajili ya kuimarisha Idara ya Mipango Miji na kusema magari hayo yatumike vizuri na kuhakikisha mpango kabambe wa jiji la Dodoma uliozinduuliwa na Waziri Mkuu Mhe. Kasim Majaliwa hivi karibuni unatekelezwe kwa vitendo.
Alitoa maelekezo hayo wakati akikabidhi magari hayo kwa Mkuu wa Idara ya Mipango Miji ya Halmashauri hiyo Joseph Mafuru katika Ofisi za Halmashauri hiyo leo Machi 18, mwaka huu.
Halmashauri ya Jiji la Dodoma imenunua magari matatu kwa thamani ya Millioni 345 kutoka katika mapato yake ya ndani ya Jiji hilo kwa ajili ya Idara ya Mipango Miji ambayo yataimarisha kitengo cha usimamizi na udhibiti wa ujenzi holela.
Awali akitoa maelezo kuhusu magari hayo kwa Mkuu wa Mkoa Dkt. Mahenge, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Godwin Kunambi alisema kuwa “Tumenunua magari matatu yenye thamani ya shilingi Milioni 345, ambapo magari mawili kila moja ni shilingi milioni 92 na gari la tatu ni shilingi milioni 160.
“Magari yote haya yatafanya kazi ya kuhakikisha Halmashauri inadhibiti kabisa ujenzi holela na kusimamia Mpango Kabambe wa Jiji la Dodoma ambao tumekabidhiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kasim Majaliwa hivi karibuni kwa ajili ya utekelezaji” alisema Kunambi.
Baada ya makabidhiano, magari hayo yalianza kazi mara moja huku kikosi kazi kinachohusika na zoezi la usimamizi na udhibiti wa ujenzi holela kikipewa rai kufanya kazi kwa bidii kwa kutowaonewa wananchi.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.