MAKUMBUSHO ya Taifa la Tanzania imepongezwa kwa uhifadhi endelevu unaowapatia wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi elimu ya masuala ya uongozi, historia na utamaduni wa Watanzania na kuifanya Taasisi hiyo iendelee kuwa kitovu cha kujifunza masuala mbalimbali.
Pongezi hizo zimetolewa na viongozi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Utold Foundation kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na zile zilizo nje ya Jumuiya hiyo wapatao 300 walioitembelea Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni iliyoko jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali kuhusu uongozi, historia na utamaduni.
Akizungumza kwa niaba ya viongozi hao, mratibu wa safari hiyo Donald Mbeke ameeleza kuwa viongozi hao wameitembelea Makumbusho hiyo ili wajifunze historia na mchango wa Taifa la Tanzania ndani na nje ya Bara la Afrika.
"Tumeona Makumbusho ya Taifa ni sehemu sahihi ya kuwaleta wageni wetu ili waweze kujifunza masuala ya uongozi, historia ya nchi yetu na utamaduni wetu, nilikua sijafika katika eneo hili kwa muda mrefu, nimekuta mambo yamebadilika sana. Mratibu huyo ameushukuru uongozi wa Makumbusho ya Taifa kwa namna ulivyowapokea na kuwapatia huduma rafiki kwa kila mmoja akiahidi kurudi kwa awamu ya pili.
Afisa Elimu Mwandamizi wa Makumbusho ya Taifa Anamery Bagenyi amemshukuru Mratibu wa safari hiyo kwa kuichagua Makumbusho ya Taifa kama sehemu sahihi ya kutembelewa na kujifunza huku akitoa wito kwa Mashirika mengine ya Kiserikali na yasio ya Kiserikali kuiga mfano wa Shirika hili la Utold Foundation.
"Makumbusho ya Taifa ni sehemu sahihi sana kwa kujifunza historia ya nchi lakini pia zipo kumbi ambao wanaweza kufanyia mikutano mbalimbali"
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.