SERIKALI imeanza ujenzi wa uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Dodoma ikiwa ni utekelezaji wa mpango wake wa kulijenga Jiji la Dodoma ili liwe la kisasa.
Kauli hiyo ilitolewa na Rais wa awamu ya sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan alipokuwa akiwahutubia mamia ya wananchi wa Dodoma na mikoa ya jirani waliojitokeza katika hafla ya uzinduzi wa mkakati wa uelimishaji na uhamasishaji wa Sensa ya watu na makazi katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma leo.
Rais Samia alisema “mmesikia hapa pia kwamba ujenzi wa kiwanja kipya cha Ndege cha kimataifa cha Dodoma. Jana mkataba wake umesainiwa rasmi. Serikali pia imeanza awamu ya pili ya ujenzi wa majengo ya wizara mbalimbali kwenye Mji wa Serikali kule Mtumba. Kila wizara itapatiwa kiasi cha shilingi bilioni za kutosha kwa ajili ya ujenzi wa majengo hayo, kuanzia ghorofa moja na kuendelea wanavyoweza huko juu kwa kiwango cha fedha watakachopewa na kuendana na mahitaji yao”.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati kuu ya Taifa ya Sensa ya watu na makazi, Kassim Majaliwa alisema kuwa jukumu la kusimamia sensa ya watu na makazi limepewa ofisi ya waziri mkuu kwa Tanzania bara. “Kwa upande wa Zanzibar Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini ya Kamati kuu ya Taita ya Sensa ya Watu na makazi inayoongozwa na Waziri Mkuu pamoja na Makamu wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar” alisema Majaliwa.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.