Na. Dennis Gondwe, DODOMA
UMOJA wa Wanawake wa Tanzania, Mkoa wa Dodoma (UWT) imefanya ziara ya kuhamasisha usawa wa kijinsia na urejeshaji mikopo inayokopeshwa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa makundi ya wanawake wajasiriamali.
Kauli hiyo ilitolewa na Mjumbe wa Halmashauri ya CCM Wilaya ya Dodoma, Jamila Mdee alipoongelea ziara hiyo katika uwanja wa michezo wa Jamhuri jijini hapa.
Mdee alisema kuwa ziara ya UWT Mkoa wa Dodoma katika Wilaya ya Dodoma ni ziara ya kawaida inayolenga kuwashukuru wajumbe kwa kuwachagua pamoja na kukumbushana masuala ya uwajibikaji. “Ziara hii inakutanisha wajumbe wa Baraza la UWT Wilaya ya Dodoma. Wajumbe watakumbushwa juu ya ulipaji wa ada za UWT, kadi za kieletroniki, mikakati ya kuongeza wanachama na kuzungumzia masuala ya unyanyasaji kijinsia. Bahati nzuri tunao wenzetu kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma ambao watatoa mada juu ya umuhimu wa mikopo ya Halmashauri kwa wanawake na urejeshaji wake ili iendelee kuwanufaisha wanawake wengi zaidi. Mada hii ni muhimu kwa sababu wanufaika wengi ni wanawake” alisema Mdee.
Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) ulianzishwa mwaka 1962 Mwenyekiti wake wa kwanza akiwa Bibi Titi Mohammed kwa lengo la kuwakomboa wanawake kifikra, kiuchumi na kisiasa.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.