WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ametoa maagizo wakati akizindua Mpango Kabambe wa Jiji la Dodoma, ambao utekelezaji wake katika miradi iliyopo na ijayo, utagharimu takribani Sh trilioni 4.1.
1. Jiji la Dodoma kwa kushirikiana na Tamisemi, wanatakiwa kutekeleza Mpango Kabambe kama unavyoelekeza kwa maendeleo ya jiji na makao makuu ya serikali.
2. Jiji la Dodoma, linatakiwa kupima viwanja kwa kasi kubwa zaidi ili kuendana na kasi ya ongezeko la watu (ili uepusha kupata ujenzi holela).
3. Jiji la Dodoma wanatakiwa kufanya mapitio ili kasi ya upimaji wa viwanja, itanguliwe na ufikishaji wa miundombinu mbalimbali katika maeneo hayo ikiwemo maji, umeme, barabara na huduma nyingine na uboreshaji wa mitaa na uwekeji taa barabarani.
4. Mkurugenzi wa Jiji, anatakiwa kufuatilia kwa karibu na kufanya tathmini ya ujenzi wa jiji kwa mujibu wa Sheria ya Mipango Miji Namba 14 (3) ya mwaka 2007 ili kupata makazi bora.
5. Jiji la Dodoma linatakiwa kutangaza fursa za viwanja katika mitandao mbalimbali, kwa kutumia pia vyombo vya habari na taasisi nyingine ili kupata huduma hizo jijini hapo.
6. Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) liongeze kasi ya kusambaza umeme katika maeneo mbalimbali. (Alitoa mfano kuwa kumekuwa na malalamiko ya kutozwa nguzo kwa wakazi wa maeneo ya Makulu, Mkalama, Nala na mengineyo na kwamba tangu mwaka jana Desemba wamelipa lakini umeme bado).
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.