Na. WAF, Morogoro
Wataalam wa afya kutoka Halmashauri mbalimbali nchini wametakiwa kutumia ujuzi waliopata kwenye mafunzo ya usalama wa maji ya kunywa kwa kuchukua na kupima sampuli za maji ili kusaidia jamii kujikinga na magonjwa ya mlipuko hasa yanayosababishwa na maji ya kunywa.
Hayo yamebainishwa leo Julai 18, 2025 na Afisa Afya Mazingira Mwandamizi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Bw. Sasita Shabani wakati wa kufunga mafunzo hayo rasmi yaliyofanyika kwa siku tatu mkoani Morogoro.
Amesema wataalam hao wanatakiwa kuzingatia lengo la mafunzo hayo na kutimiza wajibu wao wa kulinda afya za wananchi hasa kwenye maji ambayo ndiyo msingi mkubwa kwenye maisha ya kila siku.
Kwa upande wake Mkuu wa Sehemu ya Chakula Salama, Maji Salama na Usafi wa Mazingira kutoka Wizara ya Afya, Bw. Anyitike Mwakitalima, amewaasa wataalam wa afya waliopata mafunzo ya jinsi ya kupima na kugundua sampuli za maji kuhakikisha wanatumia elimu hiyo kwa vitendo katika maeneo yao ya kazi ili kutimiza lengo la Serikali la kutoa mafunzo hayo.
Naye, Afisa Afya Mazingira mkuu Wizara ya Afya Mariam Mashimba, amewasihi wataalam waliopata mafunzo hayo kujua umuhimu wa kuandaa ripoti ambayo itasaidia wakati wa uchukuaji sampuli kwa kuhusisha vyanzo vyote vya maji vitakavyochukuliwa eneo husika ili kugundua kata zinazotumia vyanzo vya maji visivyo salama na idadi ya watu wanaoathirika kwa takwimu sahihi.
Kwa upande wake Mteknolojia Maabara Hospitali ya Rufaa Morogoro Herieth Goodluck ambaye pia ni mnufaika wa mafunzo hayo, amewakumbusha wataalam wa afya kutumia nyenzo za kujilinda kama barakoa, glovu na viatu vya maji wanapokwenda kuchukua sampuli ili kujiepusha na magonjwa yanayoweza kutokea wakati wanapotimiza majukumu yao.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.