Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde amewataka vijana kutumia vyema fursa wanazozipata ili kujiingizia kipato badala ya kukaa bila shughuli yoyote na kusubiria fursa ziwafuate.
Naibu Waziri Mavunde ametoa kauli hiyo leo tarehe 24 Septemba 2019, wakati wa kukabidhiwa pikipiki 30 za usambazaji bidhaa zenye thamani ya zaidi ya TSh. 108,000,000 kutoka Kampuni ya RoutePro na kuzikabidhi kwa vijana 30 kutoka mikoa mitano ya Dar es salaam, Arusha, Singida, Mwanza na Dodoma.
“Katika kukabiliana na ukosefu wa ajira kwa vijana, serikali itaendelea kushirikiana na wadau wanaoonesha nia ya kusaidia kubuni mipango endelevu ya kuwezesha ajira kwa vijana kama ilivyofanya Kampuni ya Route Pro kwa kutoa mafunzo ya biashara kwa vijana wetu. Fursa hii ambayo imewezesha mpaka sasa Vijana 400 wameshakabidhiwa pikipiki na kujiajiri wenyewe" amesema Mavunde.
Naye Ndugu Jaja Mbazila Meneja Uratibu wa Kampuni ya Route Pro akizungumza katika zoezi hilo amesema, kampuni hiyo imepata walengwa wa kushirikiana nao katika mpango huu.
Hii imetokana na rekodi ya vijana ambao imewahi kufanya nao kazi katika miradi mbalimbali ya usambazaji bidhaa katika siku za nyuma.
Kampuni ya Route Pro imepanga kuwawezesha vijana wenye bidii ya kazi na kujituma kupata fursa kuwa na biashara zao, tumefanya nao kazi kwa karibu katika miaka iliyopita na wameonesha kuwa na nia ya kufanya vizuri biashara ya usambazaji.
Mbali na kuwapatia pikipiki, RoutePro itawapatia vijana hao kiasi cha shilingi 100,000 kila mmoja ziwasaidie kuanzia kazi na baada ya miezi 24 pikipiki hizo zitakuwa mali yao kwa ajili ya kuwasaidia katika shughuli za usambazaji ingawa watakaopenda kufanya kazi katika mpango huu wa Route Pro wa kuwezesha vijana watajiunga tena katika mpango wa miaka 2 na kupatiwa tena tena pikipiki mpya.
Tazama picha za matukio yaliyojiri wakati wa makabidhiano.
Chanzo: Dodoma_Zone
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.