KIKUNDI cha vijana cha TUSUMUKE kimepongezwa kwa uamuzi wao wa kujiunga pamoja na kubuni mradi wa kutotolesha vifaranga na kufuga samaki katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Pongezi hizo zilitolewa na mjumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Selemani Zeddy baada ya Kamati hiyo kutembelea shughuli zinazotekelezwa na kikundi hicho jana.
Zeddy alisema “napenda kuwapongeza vijana hawa kwa kujumuika na kubuni shughuli ya kufanya, hili ni jambo bora sana”. Aidha, aliwataka kuhakikisha wanarudisha marejesho ya mkopo waliopewa kwa wakati.
Kwa upande wake mjumbe mwingine, Abdallah Chikota alikisisitiza kikundi hicho kuzingatia kanuni za ufugaji bora na kuzuia magonjwa kwa vifaranga vya kuku. Alisema kuwa ni muhimu kuzingatia kanuni katika chakula, vifaranga, chanjo na huduma zote zinazotakiwa katika kanuni bora za ufugaji.
Nae Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi alisema kuwa Halmashauri yake imejipanga katika kuwajengea uwezo vijana hao na mazingira bora zaidi ya kufanyia shughuli zao. Alisema kuwa Halmashauri imetenga maeneo kwa ajili ya shughuli za vikundi vya vijana katika kata ya Nala ili waweze kutekeleza majukumu yao katika hali bora zaidi.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.