OR-TAMISEMI
Vikundi vya sanaa kutoka mikoa mbalimbali nchini vimeendelea kuonyesha uwezo wao katika fani za uimbaji na kucheza ngomo kwenye mashindano ya Umoja wa Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) yanayoendelea mkoani Tabora.
Mashindao ya sanaa za michezo yalianza kwa kushindana kwenye kwaya kabla ya leo Juni 21, 2024 kushindana katika fani ya ngoma za asili ambayo itahitimisha kesho na kumpata mshindi wa kitaifa.
Kwa upande wa fani ya muziki wa kizazi kipya maarufu kama Bongo Flavour nao unapewa nafasi kwenye mashindano ya mwaka huu, ambapo vijana mbalimbali wanatarajiwa kuonesha vipaji vyao kuanzia Juni 23, 2024 ili kupatikana kwa mshindi katika eneo hilo.
Wakati burudani ushindani katika sanaa ukiendelea kwenye ukumbi wa shule ya Sekondari Wavulana Tabora, kwingineko viwanja vya michezo mbalimbali zileiendelea kutumia vumbi katika michezo ya mwishoni ya hatua za makundi.
Mashindano ya UMISSETA 2024 yanayofanyika Mkoani Tabora kwa mwaka wa tatu mfululizo, yanaandaliwa na kuratibiwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI, ikishirikiana na Wizara ya Utamaduni Sanaa na michezo, na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia.
Kaulimbiu ya mashindano ya mwaka huu inasema “Tunajivunia mafanikio katika sekta ya elimu, Michezo na Sanaa, Hima Mtanzania shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024”
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.