• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Vilabu vya michezo vyashiriki mazoezi ya viungo vya mwili jijini Dodoma

Imewekwa tarehe: February 24th, 2025

Na. Aisha Ibrahim, CHAMWINO

Vilabu mbalimbali vya michezo jijini Dodoma, vimejitokeza kwa wingi katika Bonanza la “Dodoma Aerobics Festival” msimu wa kwanza, lililofanyika katika kiwanja cha Chinangali Park, kuanzia saa 12:00 asubuhi mpaka saa 6:00 mchana kwa lengo la  kuwakutanisha wanamichezo wote kushiriki mazoezi mbalimbali ya kuimarisha viungo vya mwili.

Bonanza hilo liliandaliwa na kikundi cha wakufunzi wa michezo kutoka Jiji la Dodoma 'Dodoma Trainers Group' lilijumuisha mchezo wa kunyanyua uzito, kupasha mwili, kurukaruka na vikundi vya kukimbia.

Akizungumza wakati wa bonanza hilo, mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri, aliwasisitiza wana Dodoma kuendelea kufanya mazoezi kila siku hasa siku ya Jumamosi kama ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, alivyosisitiza kila mtanzania kujitengea siku ya kufanya mazoezi kwa lengo la kuimarisha viungo vya mwili. “Mazoezi ni afya, mazoezi ni tiba hivyo, nawapongeza sana waandaaji wa “Dodoma Aerobics Festival” kwa kuja na hiki kitu muhimu Jiji la Dodoma na kutambua umuhimu wa michezo” alisema Alhaj Shekimweri.

Aliongeza kuwa, ushiriki wa mazoezi mbalimbali huleta fursa ya watu kutoka maeneo tofauti kukutana na kujumuika kwa pamoja katika kuburudika na kubadilishana uwezo na uwelewa wa mambo mbalimbali yanayohusiana na michezo. "Mazoezi yana tafsiri nyingi na nikisema hivi najua wana mazoezi wananielewa kwasababu kijamii kujichanganya huleta fursa ya kukutana na marafiki na viongozi mbalimbali kuburudika nao na kubadilishana mawazo na uelewa wa masuala ya kimichezo” alisema Alhaj Shekimweri.

Kwa upande wake, Afisa Habari wa “Dodoma Aerobics Festival” Emmanuel Juma, alisema kuwa wanajivunia kuanzishwa kwa tamasha kubwa la kuwakutanisha wana mazoezi kutoka vilabu mbalimbali na kupata fursa ya kujumuika kwa pamoja kufanya mazoezi ya kuimarisha viungo vya mwili. “Hili ni tamasha ambalo limekusanya vilabu vyote vya 'jogging' na wafanya mazoezi kutoka vituo mbalimbali Jiji la Dodoma lakini pia wapo wengine wametoka Wilaya ya Bahi, Mkoa wa Morogoro, Mkoa wa Tabora na mikoa tofauti tofauti. Hivyo, nijivunie kuwa hili ni tamasha kubwa na la Kipekee hapa jijini Dodoma” alisema Juma.

Nae, mwalimu kutoka kituo cha kufanyia mazoezi “Home Fitness Center” kilichopo Kata ya Nzuguni, Ally Lwambo, alifafanua kuwa kila mtu ana wajibu wa kufanya mazoezi ya viungo vya mwili kila siku bila kuzingatia suala la unene au wembamba wa mwili ili kujenga ukakamavu na uwezo mzuri wa kufikiria. “Ni wajibu wa kila mtu kufanya mazoezi kwasababu mazoezi ni afya na hayana mwembamba wala mnene hivyo ukipata muda wowote wa kufanya mazoezi basi shiriki ipasavyo” alisema Lwambo.

Sambamba na hayo, mmoja kati ya washiriki wa mazoezi hayo Acxa Madinda, alishauri kuwa mazoezi hayo yasiishie kwa watu wazima badala yake hata watoto waandaliwe matamasha mbalimbali ya michezo ya kuimarisha viungo vya mwili kwasababu michezo ni kujifunza na kuburudika. “Kama mnavyoona mimi nilikuja na mtoto wangu na baada ya kufanya mazoezi amefurahi sana hivyo nìshauri haya matamasha yasiishie tu kwa watu wazima bali yaandaliwe hata kwa watoto ili nao waweze kuburudika” alisema Madinda.

Kufanya mazoezi ya mwili kuna faida nyingi muhimu kwa afya ya mtu kama vile husaidia kudhibiti uzito wa mwili, kusaidia kuondoa mafuta yasiyohitajika mwilini, kuimarisha misuli na mishipa husaidia kuboresha hali ya akili na kufikiri.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.