VIONGOZI wa nchi tatu za Uganda, Comoro na Zimbabwe na wengine wapatao 20 pamoja na mabalozi 83 wanaowakilisha nchi zao hapa nchini wamethibisha kuhudhuria sherehe za kuapishwa Rais wa Tanzania.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas (pichani juu) amesema hayo leo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jijini Dodoma leo kuhusiana na maandalizi ya hafla ya kumuapisha Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, itakayofanyika kesho Novemba 5, 2020 katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Aidha Dkt. Abbas amesema maandalizi yamekamilika na hafla hiyo itahudhuriwa na mbalimbali takribani 20 wakiwemo Marais watatu kutoka Uganda, visiwa vya Comoro na Zimbabwe, Makamu ya Rais wa Nchi kadhaana mawaziri wakuu wa nchi kadhaa wakiwemo pia viongozi wengine mashuhuri kama Rais mstaafu wa Nigeria Olussegun Obasanjo, Nabii T.B. Joshua, Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar, vilevile amesema mabalozi 83 wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini watahudhuria pia.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.