VIONGOZI na Wataalam wa Elimu Mkoa wa Dodoma wamepitisha Rasimu ya Mkakati wa Elimu Mkoa wa Dodoma 2024 baada ya kutamatika kwa Kikao Kazi Maalum kilichowakutanisha Wataalam na Viongozi kwa Muda wa siku 4 katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Ualimu Bustani Wilayani Kondoa tarehe 08/12/2023.
Kikao Kazi hicho kimefungwa na Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule baada ya kupokea taarifa ya kilichojadiliwa kwa kipindi chote na kikao Kazi hicho kwa kufanya Tathmini ya pamoja ya Maendeleo ya Elimu, kuruhusu Majadiliano ya pamoja na Kisha kuipitisha Rasimu hiyo ya Mkakati wa Elimu Mkoa wa Dodoma 2024.
Senyamule ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuwaletea Maendeleo Watanzania kwenye Sekta ya Elimu na kwa Mkoa wa Dodoma katika kipindi cha mwaka 2022/23 na 2023 /24 ambapo hadi sasa Dodoma imepokea Sh Bil. 73 Mil 522 na Elfu 30 kwa ajili ya Ukamilishaji Miundombinu ya Madarasa, Nyumba za Walimu, Matundu ya Vyoo, Mabweni ya wanafunzi, Majengo ya Utawala, Mabwalo, Uzio wa Mabweni ya Watoto wenye Mahitaji Maalum, Maabara pamoja na Vituo vya TRC.
"Kuwepo kwa Miundombinu hii imesaidia kiasi kikubwa kupunguza Wanafunzi kutembea Umbali Mrefu kufuata huduma ya Elimu, Msongamano wa Wanafunzi Madarasani, Utoro, uwepo wa Mazingira salama na rafiki kwa Wanafunzi na sote ni Mashahidi kuwa Rais ni Mahiri na Amefanya haya kwa dhamira yake thabiti katika Uongozi wa Serikali ya Awamu ya 6,"amesema Senyamule.
Senyamule ametumia nafasi hiyo kupongeza Uandaaji na kufanyika kwa kikao hicho na kuja na ubunifu ili kwenda na kasi zaidi ili ubora wa Elimu uendane na hadhi ya Mkoa wa Dodoma kama Makao Makuu ya nchi na Chama Tawala.
Vivyo hivyo kwa Upande wa Wakuu wa Wilaya, Mstahiki Meya wa Jiji la Dodona pamoja na Wenyeviti wa Halmashauri za Mkoa wa Dodoma wamepongeza jitihada za kuandaliwa kwa Mkakati huo wa Elimu Mkoa 2024 wakiwa na matumaini ya Kama mkakati huo Ukitumika vyema utaongeza kasi ya ufaulu kwa wanafunzi na kuahidi kufanyia kazi Mkakati huo kwa kuanzisha Mfuko wa Elimu utakaosaidia kukuza Sekta ya Elimu Mkoa wa Dodoma.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.