VIONGOZI wa Wilaya na Halmashauri ya Jiji la Dodoma leo wameungana na wakazi wa Kata za Kikuyu Kaskazini na Kikuyu Kusini katika muendelezo wa kampeni ya USAFI WA Mazingira na utatuzi wa kero za wananchi kwa mtindo wa Kata kwa Kata.
Viongozi hao wakiongozwa na Mkuu wa wilaya Jabir Shekimweri na kamati yake nzima ya ulinzi na usalama ya wilaya walishirikiana na wakazi wa kata hizo kufyeka vichaka, nyasi na kusafisha mitaro ikiwa ni juhudu za wilaya kuhakikisha Makao Makuu ya Nchi hasa Jiji la Dodoma linakuwa safi muda wote.
Akizungumza na wakazi hao, Mkuu huyo wa Wilaya aliwataka kufanya usafi kuwa ni tabia na ada ya kila siku ikihusisha ndani nan je ya nyumba pamoja na sehemu za kazi kama maeneo ya biashara na maeneo ya wazi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Joseph Mafuru aliwaeleza wananchi wa Kata hizo kuwa Halmashauri imedhamiria kupendezesha Makao Makuu ya Nchi kwani ndiyom jicho la nchi na kwamba kila mwananchi ana wajibu wa kuhakikisha hachafui mazingira yake wala ya mwenzake.
Mkurgenzi Mafuru alisema Jiji linaandaa utaratibu wa kuhakikisha kuwa, kila mwananchi anakuwa mlinzi wa mwenzake katika kusafisha na kutunza mazingira ambapo mtu akayemripoti mchafuzi wa mazingira atalipwa nusu ya fedha za faini atakazotozwa aliyechafua mazingira.
Alisema utaratibu huo utatekelezwa katika Jiji hilo hivyo kila mkazi awe makini na kuacha kutupa taka hovyo zikiwemo vocha za muda wa maongezi wa simu kwani atakayekamatwa atatozwa faini inayoanzia shilingi 50,000 hadi 300,000 kwa mujibu wa sheria za mazingira kulingana na aina ya uchafuzi ulioufanya.
Naye mkuu wa idara ya Mazingira wa Jiji hilo Dickson Kimaro alisema kampeni hiyo ni endelevu na kwamba kila Jumamosi ya kila wiki viongozi hao wakuu ngazi ya wilaya watajumuika na wananchi wa kata mojawapo itakayotangzwa baadaye na kufanya nao usafi kwa lengo la kuhamasisha na kuonesha mfano huku pia wakisikiliza kero za wakazi husika na kuzitolea majibu.
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Joseph Mafuru akizungumza na Wakazi wa Kata ya Kikuyu Kaskazini wakati wa kampeni ya usafi wa mazingira katika iliyofanyika katika kata hiyo Januari 29, 2022 ambapo zoezi hilo lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa ngazi ya wilaya akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri Mkuu wa Wilaya Jabiri Shekimweri akishiriki zoezi hilo la usafi wa mazingira Baadhi ya wakazi wa Kata ya Kikuyu Kaskazini wakishiriki usafi huo, nyuma ni magari yanayotumika kubebea taka
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Joseph Mafuru akizungumza na Wakazi wa Kata ya Kikuyu Kusini wakati wa kampeni ya usafi wa mazingira katika iliyofanyika katika kata hiyo Januari 29, 2022 ambapo zoezi hilo lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa ngazi ya wilaya akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.