Halmashauri ya Jiji la Dodoma imepokea jumla ya vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo 5000 vilivyotolewa na Rais Dkt. John Magufuli kwa lengo la kuwatambua na kuwawezesha kufanya biashara kwa uhuru bila kusumbuliwa na mamlaka nyingine za kodi.
Akizungumza wakati wa kupokea vitambulisho hivyo kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Patrobas Katambi amesema wanaandaa utaratibu mzuri utakaotumika kugawa vitambulisho hivyo kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji la Dodoma bila usumbufu kwa wafanyabiashara hao.
Vitambulisho hivyo vinatolewa kwa gharama ya shilingi elfu ishirini kwa kila kitambulisho na wafanyabiashara wanaokidhi vigezo vya kupata vitambulisho hivyo ni wale wenye mzunguko wa kibiashara usiozidi shilingi milioni nne kwa mwaka na wasiwe wameshawahi kupatiwa namba ya utambulisho wa Mlipakodi yaani TIN ya kibiashara hapo awali.
Pichani Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge (wa kwanza kushoto) akikabidhi boksi lenye vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo kwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Patrobas Katambi (katikati) na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi (kulia). Shughuli hii imefanyika Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.