NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - TAMISEMI anayeshughulikia Afya Dkt. Grace Magembe amesema Serikali inaendelea kuhakikisha vituo vya kutolea huduma za Afya ya msingi nchini vinaendelea kufungwa mfumo wa kielektroniki wa kudhibiti na kufuatilia taarifa za mteja (GoTHoMIS).
Dkt. Grace ameyasema hayo wakati wa hafla makabidhiano ya vifaa vya TEHAMA 8vya (GoTHoMIS) katika vituo vya kutolea huduma za Afya katika Mkoa wa Dodoma
Amesema kwa mkoa wa Dodoma jumla ya Vituo 235 vya kutolea huduma za afya vinatarajiwa kunufaika na vifaa hivyo vilivyotolewa na Serikali ya Korea kupitia Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Korea (KOICA) linalotekeleza mradi huo Mkoani Dodoma
“mfumo unatusaidia kuondoa ukilitimba pamoja kupata takwimu sahihi na kuongeza ufanisi wa kazi zetu hasa katika sekta ya Afya Ofisi ya Rais TAMISEMI inahakikisha vituo vyetu vyote kuanzia hospital za wilaya vituo vya Afya na zahanati sasa hivi wanatoa huduma kwa kutumia mifumo" amesema Dkt.Grace
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amewaelekeza waganga wakuu wa Halmashauri za mkoa wa Dodoma kuhakikisha wanatunza vifaa vinavyowezesha kuongeza ukusanyaji wa mapato, kufuatilia na kudhibiti taarifa za mgonjwa.
"Vituo 135 vitapata vifaa hivi vikiambatana na usimikaji pamoja na mafunzo kwa watumiaji, vituo 82 vitapewa vifaa pekee hivyo, Wakurugenzi hakikisheni vifaa hivi vinasimikwa na kuanza kutumika ili tusipoteze dhamira ya waliotuwezesha” anaeleza
Vilevile, Mkurugenzi Mkazi wa KOICA Bw. Man Sik Shin amesema Serikali ya Korea Kusini inashirikiana na Tanzania kwenye utekelezaji wa miradi ya sekta za elimu na afya ambapo Mradi huo umegharimu zaidi ya Bilioni 16.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.