Na. Dennis Gondwe, DODOMA
HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imetoa viwanja mbadala 1,105 kwa wananchi katika kutekeleza mkakati wake wa kumaliza migogoro ya Ardhi jijini hapa.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, John Kayombo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa Kliniki ya Ardhi iliyo katika siku yake ya pili ya kutatua migogoro ya Ardhi jijini hapa.
Kayombo alisema kuwa wakati anafika Dodoma kulikuwa na wananchi takribani 4,000 wanaodai viwanja mbadala. “Yaani kiwanja kimoja kimegawiwa kwa mwananchi zaidi ya mmoja. Lakini mpaka sasa tumeshatoa viwanja 1,105 kufidia wale wananchi. Mpaka sasa tunadaiwa viwanja 2,895. Matarajio mpaka kufikia mwezi Desemba mwaka huu tutakiwa tumekamilisha kutoa viwanja hivyo 2,895. Kwa sababu kuna zoezi kubwa linaendelea la kupima eneo la Mahomanyika viwanja vitapatikana 7,000 na tutaoa viwanja 2,895 na kuwapatia wananchi viwanja vyao” alisema Kayombo.
Kliniki ya Ardhi imewaweka pamoja wataalam wote wa sekta ya Ardhi ili kupokea, kusikiliza na kutatua migogoro ya Ardhi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.