• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Vyama vya siasa vyapongezwa kudumisha Demokrasia jijini Dodoma

Imewekwa tarehe: November 21st, 2024

Na. Faraja Mbise, DODOMA

Vyama vya siasa katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma vimepongezwa kwa kuonesha ushirikiano mkubwa kuanzia mchakato wa uandikishaji wa orodha ya wapiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mpaka hatua ya kampeni za uchaguzi kwa wagombea mbalimbali.

Hayo yalisemwa na Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Frederick Sagamiko alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari pamoja na viongozi wa vyama vya siasa ofisini kwake.

Dkt. Sagamiko alivipongeza vyama vya siasa kwa ushirikiano mkubwa waliouonesha katika michakato yote ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuanzia kujiandikisha katika orodha ya wapiga kura, kuchukua na kurejesha fomu za kugombea uongozi, pingamizi kuhusu uteuzi mpaka zoezi linaloendelea la kampeni za uchaguzi.

“Ndugu zangu, baada ya kukamilisha zoezi la uandikishaji, ambapo ninyi wadau wa uchaguzi, viongozi wa vyama vya siasa na waandishi wa habari na wananchi kwa ujumla, sisi Jiji la Dodoma tunapoenda tarehe 27 Novemba, 2024 tunatarajia kuwa na wapiga kura 628,715. Kati yao wanaume ni 312,850 na wanawake ni 315,865. Kwahiyo, hawa ndio wapiga kura tunaowatarajia. Na hao ndio waliopo katika madaftari yetu baada ya michakato yote ikiwemo kuwekea mapingamizi wale waliojiandikisha, hawa ndio waliobaki kwenye madaftari yetu. Watu hawa wanaenda kupiga kura na kupata viongozi wao wanaotoka kwenye jumla ya vyama vya siasa 14, tukumbuke kuwa, tuna vile vyama vyenye usajili wa kudumu 19 na mnakumbuka vyama vyote vilichukua fomu, vyama vitano havikurejesha. Sasa tunapoelekea tarehe 27 hao tunaoenda kuwapigia kura wanatokana na vyama 14 vya siasa. Naomba nirejee vyama hivyo kwa ajili ya kumbukumbu, vyama hivyo ni pamoja na; CCM, CHADEMA, ACT WAZALENDO, NCCR MAGEUZI, UDP, AAFP, CCK, UMD, ADA-TADEA, MAKINI, TLP, NLD, UPDP na SAU. Hapa ndio jumla ya vyama 14, kiupekee sisi wana Dodoma tunajivunia ushiriki wa vyama vya siasa katika kudumisha demokrasia yetu. Naomba nitoe pongezi sana kwa viongozi wa vyama vya siasa” alisema Dkt. Sagamiko.

Akitoa takwimu za wagombea wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kuhusu kampeni za wagombea wa vyama vya siasa zilizofunguliwa rasmi tarehe 20 Novemba, 2024 na kudumu ndani ya siku saba kabla ya uchaguzi, Msimamizi wa Uchaguzi alivitaka vyama vya siasa kuzingatia muda sahihi wa kuanza kampeni hizo na kufuata kanuni na taratibu ili kufanya uchaguzi wa kidemokrasia.

“Baada ya kujua idadi ya wapiga kura na vyama vinavyoshiriki, naomba nirejee pia idadi ya wagombea, kwa nafasi ya wenyeviti wa mitaa jumla ya wagombea 326 watashiriki, kwa upande wa wajumbe tuna wajumbe mchanganyiko na wajumbe kundi la wanawake. Jumla ya wajumbe mchanganyiko watakaogombea ni 799 wakati wajumbe wanawake ni 458. Kwa Jiji la Dodoma nafasi hizo za wenyeviti wanagombea mitaa 222 na wajumbe mchanganyiko Mitaa 221 lakini wajumbe wanawake ni mitaa 222. Naomba kuchukua nafasi hii kuwakumbusha kwamba, kwa mujibu wa kanuni zetu kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 zitaanza saa 02:00 Asubuhi na kumalizika saa 12:00 Jioni kila siku ya kampeni, na kampeni zetu zitakoma tarehe 26 Novemba, 2024 saa 12:00 Jioni” alisisitiza Dkt. Sagamiko.

Katika kuhakikisha zoezi la kampeni za wagombea mbalimbali wa vyama vya siasa linakuwa la amani na kidemokrasia, Msimamizi wa Uchaguzi aliwakumbusha viongozi wa vyama vya siasa kufuata kanuni wakati wa kampeni zao ili kuepukana na vurugu wakati wa mchakato huo.

“Naomba niwakumbushe viongozi wa vyama vya siasa, wakati wote wa kampeni yapo mambo ambayo haturuhusiwi kufanya kwa mujibu wa kanuni zetu tulizojiwekea na kuridhia sisi wenyewe. Moja, kutoa maneno yanayolenga uvunjifu wa amani au kuchochea vurugu, tunaomba sana muwakumbushe wagombea wenu wajizuie kutoa maneno yanayoleta uvunjifu wa amani au kuchochea vurugu. Pili, kutumia rushwa, watu kutafuta mamlaka kwa njia ya rushwa, tatu kutoa maneno ya kashfa na matusi kwa chama fulani au mgombea fulani. Nne, kutumia ubaguzi mfano wa jinsia, dini au kabila lake” aliongea Dkt. Sagamiko.

Aidha, aliwataka wananchi wote wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, kuhudhuria katika kampeni za wagombea wa uenyekiti na wajumbe ili waweze kuzielewa sera za wagombea kama zinamanufaa kwa maendeleo ya mitaa wanayoishi na ifikipo siku ya kupiga kura wafanye maamuzi sahihi ya kuchagua kiongozi bora.

Dkt. Sagamiko alisema “nitoe rai kwa wananchi wote wa Jiji la Dodoma, tuweze kujitokeza kwa wingi kufuatilia, kushiriki kwenye hizo kampeni, tusikilize sera za wagombea mbalimbali wa vyama vyote vya siasa 14 vilivyoomba nafasi mbalimbali katika Jiji letu la Dodoma ili waweze kuwapima na hatimae tarehe 27 waweze kutumia haki yao ya kikatiba kuwachagua viongozi wanaowapenda watakaoshika nyadhifa hizo kwa muda wa miaka mitano”.

Kwa kutambua mchango wa waandishi wa habari katika zoezi hili la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, aliwapongeza kwa kazi kubwa ambayo wanaifanya na kuwataka kutoa ushirikiano zaidi katika kipindi hiki cha kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

“Waandishi wa habari ninyi mna sauti kubwa inayoweza kuifikia jamii kwa muda mfupi, tushirikiane katika kuhakikisha kwamba wananchi wetu wanafikiwa na taarifa mbalimbali na sera za viongozi mbalimbali. Tunatamani sana kwenda kufanya ‘coverage’ kwenye viongozi wakubwa hasa kwenye Uchaguzi wa Serikali Kuu, lakini naomba niwakumbushe kwamba Uchaguzi wa Serikali za Mitaa una umuhimu mkubwa katika mustakabali wa maendeleo yetu ya Jiji la Dodoma. Kwahiyo wapeni nguvu na vipaumbele sawa wagombea wetu kwa nafasi mbalimbali kwenye mamlaka za serikali za mitaa” alisisitiza Dkt. Sagamiko.

MWISHO

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.