• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Vyama vya ushirika nchini vyatakiwa kujiendesha kisasa

Imewekwa tarehe: September 11th, 2021

MRAJIS wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Dkt. Benson Ndiege amevitaka vyama vya ushirika nchini, kujiendesha kisasa ikiwa ni pamoja na kuwa na ushirika wenye kugusa makundi yote, vijana, wazee kina mama na wafanyakazi wa makundi yote.

Pia, amesema wataanza kutumia mifumo ya kieletroniki katika ukusanyaji wa taarifa mbalimbali ambazo zitawasaidia kujiendesha kisasa.

Hayo ameyasema leo jijini Dodoma wakati wa kikao kazi cha wadau wa ushirika kutoka Mikoa mbalimbali nchini. Dkt. Ndiege amesema kwa sasa ni lazima kuwe na ushirika wa kisasa na kuachana na yale mazoea.

“Lazima tubadilike tuwe na ushirika ambao unawagusa vijana, wazee kina mama na wafanyakazi na makundi yote. Wavuvi, watu wa habari lazima tusibaki na ushirika wa kizamani hata mifumo yetu lazima iende kisasa. Wewe kama unaendelea kutembea na makaratasi wenzako wapo kwenye simu wanapata ‘information’ (Habari), lazima na sisi tuendane na hali halisi ya nchi yetu jinsi ilivyo,” amesema Dkt. Ndiege.

Aidha, Dkt. Ndiege amesema ili ushirika uweze kwenda vizuri ni lazima kuwe na imani kwa kile ambacho kinafanyika ambapo watu wasipokuwa na imani ni sawa na kazi bure.

“Kwa sasa tunachotamani kwa ukubwa ni imani katika vyama vya ushirika watu wasipokuwa na imani hata tupige kelele au tuweke mifumo gani hawatatumia fursa hizo.

“Hatuwezi kwenda bila kuleta imani hili ni jukumu letu sote lazima tuanze kwa kujenga imani kwa kuwa waaminifu,” amesema Dkt. Ndiege.

Amesema malengo yao ni kuhakikisha kunakuwa na vyama imara vya ushirika ikiwemo kuviona vyama hivyo vinakuwa na mifuko ya pembejeo ili viweze kujitegemea.

“Ni bora kuwa na vyama vichache na sisi tunajikita na kuwa na vyama imara vya ushirika kwa sababu hiyo tunayo malengo ambayo yatatusaidia, mojawapo kwenye vile vyama vya mazao tungependa kuona vyama hivyo vinakuwa na mifuko ya pembejeo na sisi tutajenga mazingira jambo hili liende vizuri,” amesema Dkt. Ndiege.

Vilevile, amesema lazima waanze kutoa huduma mbalimbali kwa wanaushirika ikiwemo huduma ya Bima ya afya ili wanachama waone umuhimu wa kuwa katika vyama hivyo.

“Tunataka kuona vyama vya ushirika vikitumia mifumo ya masoko ni namna gani ya kumsaidia mkulima kuweza kupata soko, Tume ya Ushirika ipo tayari kushirikiana na wadau kuhakikisha wanapata masoko,” amesema Dkt. Ndiege.

Pia, Dkt. Ndiege amesema kuna changamoto ya wizi katika vyama vya ushirika hivyo wamejipanga kwa miaka mitano ijayo kuwashughulikia wote ambao wataiba katika ushirika.

“Tumejikita zaidi kuingia katika mifumo ya kieletroniki katika vyama vya ushirika na tayari zoezi hili limeanza na tutatunza taarifa vizuri,” amesema.

Pia, vyama vya ushirika kuanzisha na kusimamia viwanda vikubwa na vidogo lengo likiwa ni kuongeza thamani za mazao nchini.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania, Theresia Chitumbi amesema Mkutano huo upo kwa ajili ya kuaandaa ushirika mpya ambao utaenda kisasa.

“Tupo hapa kuandaa mikakati ya Tume ya Ushirika kwani ni wadau wa ushirika tupo kwa ajili ya kuleta ushirika mpya na hilo ndio lengo la Rais wetu na tumeona Nchi nyingi ambazo ushirika umesimama ndio wana maendeleo makubwa,” amesema.

Amesema ushirika wa zamani ulikuwa wa mazao tu lakini sasa hivi wamejipanga kuwavuta vijana na kuubadilisha ushirika na uwe wa kidigitali.

“Mimi kwa mtazamo wangu tunatakiwa kubadilika tuwe na ushirika wa kidigitali kuliko kwenye makatarasi ukiwa kidigitali kila kitu kinaonekana tumeanza kuwaingiza vijana kwa kufanya mashindano ya insha na wameanza kuujua ushirika ni nini,” amesema.

Chanzo: Alex Sonna, DODOMA

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.