MKURUGENZI wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Godwin Kunambi ameongea na waandishi wa Habari mapema leo katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma na kutoa taarifa kwa umma wa Watanzania juu ya mabadiliko ya utoaji fomu za kuomba nafasi ya vyumba vya biashara katika miradi ya kimkakati iliyokamilisha ujezi wake katika Jiji hilo, ikiwemo Kituo Kikuu cha Mabasi na Soko Kuu la Job Ndugai.
Kutokana na uwepo wa ugonjwa wa COVID-19, tahadhari zaidi ya gonjwa hilo zinachukuliwa hivyo Halmashauri ya Jiji la Dodoma imezingatia hilo na kuanzisha mfumo wa utoaji fomu za biashara katika miradi yake ya kimkakati yaani Soko Kuu la Job Ndugai, Kituo cha Mabasi, Kituo cha Maegesho ya Malori na Eneo la Kupumzikia Chinangali, ambapo sasa fomu za maombi zitatolewa kwa njia ya mtandao kuanzia wiki ijayo.
“Utoaji wa fomu kwa njia ya kimtandao utawafikia Watanzania wote tena bila ubaguzi kabisa kwani mtu yeyote aliyepo mikoani atakua sawa na aliyepo Dodoma, mfumo huu utakamilika Jumatatu wiki ijayo na wananchi watapata fursa ya kupata fomu zao wakiwa nyumbani tena kiganjani” alisema Mkurugenzi Kunambi mbele ya Wanahabari.
Kunambi alisema mfumo huo utapunguza msongamano, utapunguza adha ya wananchi kusafiri kutoka mikoa jirani na kufungua milango kwa Watanzania wote kuwa na nafasi sawa na ya haraka, fomu hizo zitagharimu shilingi 20,000 na malipo yake yatafanyika kwa njia ya malipo mtandao, ambapo muombaji atapakua fomu mtandaoni, ataijaza, na kuirejesha huku akiwa amelipia shilingi elfu ishirini (20,000) kwa kutumia ‘control number’ ambayo pia ataipata mtandaoni sambasamba na fomu.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.