WACHEZAJI wa timu ya Dodoma Jiji FC wametakiwa kuheshimu na kutunza vipaji vyao kwani hicho ndicho kitu pekee kinacho waingizia kipato na kuwafanya waheshimike na kuendesha maisha yao.
Hayo yamesemwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma Prof. Davis Mwamfupe wakati akifungua semina maalum iliyoandaliwa na uongozi wa timu hiyo kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kujitambua pamoja na kuhafamu mambo mbalimbali yanayohusu soka la kulipwa.
Mwamfupe alisema kuwa, timu ya Dodoma Jiji ipo katika nafasi nzuri katika ramani ya soka Tanzania na hatarajii kusikia taharifa zozote mbaya zinazohusu wachezaji kwani tayari timu hiyo ni kubwa na inatazamwa kwa jicho la tofauti.
“Semina kama hizi ziwe endelevu ili kuwajenga wachezaji kisoka na kiuchumi wachezaji hawa, na kama hii ndiyo itakuwa mara ya kwanza na ya mwisho ni bora msifanye kwa sababu haitaleta maana ila kama itakuwa endelevu mtajenga timu yenye vijana waelewa na mtaacha alama hata watakapokua nje ya timu hii watawakumbuka kwa kuwajengea uwezo” alisema Meya huyo.
Semina hiyo ilihudhuriwa na viongozi wa juu wa timu hiyo, wachezaji, na benchi la ufundi ambapo muwezeshaji mkuu alikuwa ni mchezaji wa zamani wa soka wa Tanzania ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa soka Ally Mayai.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.