Na. Josephuna Kayugwa, DODOMA
MKURUGENZI wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru amewataka wachezaji wa timu ya mpira wa Mikono ya wafanyakazi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kujituma katika mashindano ya SHIMISEMITA yanayofanyika mkoani Morogoro kwasababu michezo ni afya na inatengeneza ushirikiano.
Ameyasema hayo alipokutana na timu kwa lengo la kuwatia moyo wakati wachezaji walipokuwa katika maandalizi ya kwenda Morogoro kushiriki mashindano hayo kama wafanyakazi.
“Sisi kama Jiji la Dodoma tuna furaha sana timu yetu inakwenda kushiriki mashindano na tunaamini muda huu watafanya vizuri kwenye michezo yote mitatu na watarudi na ushindi hapa Dodoma.
“Pia nimewasisitiza pamoja na kuwa wanamichezo lakini ni watumishi wacheze kwa tahadhari ili tusipate majeruhi, wawe waangalifu wasipate ajali kwenye mchezo na ninawatakia kila la kheri wachezaji wote,” alisema Mafuru.
Kwa upande wake Nahodha wa timu, Theopista Mnyang’ali alisema wamejiandaa vizuri katika mashindano ya SHIMISEMITA wamefanya mazoezi ya kutosha kama wachezaji wana imani watafanya vizuri na kurudi na ushindi.
“Tumejiandaa kikamilifu na hivi mara yetu ya kwanza kushiriki mashindano ya SHIMISEMITA naimani tutakwenda kufanya vizuri huko Morogoro na kurudi na makombe yote matatu,” alisema Mnyang’ali.
Naye Emmaculata Chale mchezaji wa timu ya mpira wa mikono, alimshukuru Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma kwa kuwaunga mkono na wameahidi kurudi na ushindi kwasababu wanakwenda kushiriki michezo mitatu.
“Tunakwenda kushiriki michezo ya SHIMISEMITA 2022, mkoani Morogoro kwahiyo tutarudi na makombe mengi tu na hatutawaangusha lakini pia shukrani kwake Mkurugenzi na tutamletea ushindi,” alisema Chale.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.