KITENGO cha Lishe katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma kimekutana na wadau kujadili utekelezaji wa mkataba wa Lishe Endelevu ngazi ya Kata ulivyotekelzwalizwa katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita yaani Julai hadi Septemba 2020.
Kikao hicho cha tathimini kilifanyika katika ukumbi mkuu wa Halmashauri ya Jiji hilo ambapo pamoja na wadau wengine, kilihudhuriwa na watendaji wa Kata ambao ndiyo wasimamizi wakuu wa shughuli za Halamshauri katika ngazi ya Kata.
Akizungumza na wadau hao, Afisa Utumishi katika Halmashauri hiyo Innocent Kessy ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wa Jiji Joseph Mafuru alisema kuwa, imefika wakati kila kaya ifikiwe na watendaji hao kuhamasishwa kulima bustani ndogo ndogo za mboga na matunda kwa ajili ya matumizi ya familia.
Kessy alisema kila mdau na taasisi ikiwemo shule zote zihamashishwe na kusimamiwa katika ngazi ya Kata ili kuongeza muamko katika jamii nzima kuhusiana na mausuala ya lishe.
Kwa upande wake, mratibu wa Lishe katika Halmashauri hiyo Semeni Juma alisema kuwa, miongoni mwa mikakati ni kusaidia masuala ya lishe kwa watoto chini miaka mitano, akina mama wajawazito, na vijana walio katika rika balehe kama makundi maalum.
Mratibu huyo alisema kwa mwaka wa fedha 2020/2021 Halmashauri ya Jiji la Dodoma imetenga shilingi milioni 83 kwa ajili ya kusimamia na kutekeleza shughuli mbalimbali za lishe.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.