NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia elimu Dkt. Charles Msonde amewataka wadau wote wanaotoa huduma za afya nchini kuhakikisha wanafanya kazi hiyo kwa utashi, uvumilivu na upendo kwa wananchi.
Ametoa kauli hiyo Oktoba 13, 2022 wakati akifunga kongamano la 9 la wadau wa afya Kitaifa, jijini Dar es salaam
Amesema kuwa utoaji wa huduma bora kwa wananchi kunahitaji uvumilivu, utashi na kujitoa kwa moyo kwa kuwa huduma hiyo ni sadaka kwa Mungu.
"Suala la kutoa huduma za afya kwa Watanzania ni Mungu mwenyewe, kumuhudumia mtu ili apate afya ni jambo la msingi kuliko kitu chochote, naomba tujitoe kwa hilo" amesisitiza Dkt.Msonde
Amesema katika miaka miwili Serikali imetumia zaidi ya shilingi bilioni 821 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya afya na kununua vifaa tiba
Ameendelea kusema kuwa jitihada hizo ni ishara kuwa Serikali imejikita katika kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma nzuri za afya kwa ajili ya kuboresha afya huku ikitambua kuboreshwa kwa afya ya mtu huwezesha sekta zote za kiuchumi kuendelea na kusimama vizuri
Amesema Serikali imehakikisha inajenga miundombinu ya kutolea huduma za afya zikiwemo zahanati 1, 122, vituo vya afya 310 na Hospitali za Wilaya 102 licha ya kujenga hospitali hizo mpya 25, ujenzi wa vituo vya dharura 80 licha ya vituo vya dharura 25 vilivyojengwa tayari.
Ameendelea kufafanua kuwa licha ya ujenzi wa miundombinu na ununuzi wa vifaa tiba, Serikali iliona upo umuhimu wa kuajiri wataalamu wa afya 10,338 wameajiriwa ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya nchini
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.