WADAU wa uwekezaji katika nyanja ya hoteli wametembelea eneo la uwekezaji la Njedengwa Jijini Dodoma mwishoni mwa wiki iliyopita ambalo pamoja na kuwa na viwanja vya ujenzi wa taasisi, pia kuna viwanja kwa ajili ya uwekezaji wa hoteli kubwa za kisasa.
Wadau hao kutoka kampuni mbalimbali na taasisi ikiwemo wawakilishi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii wamevutiwa na mradi huo wa ukanda wa uwekezaji ambao tayari umewekewa miundombinu muhimu ikiwemo umeme, maji, na barabara za lami.
Awali kabla ya kutembelea eneo hilo, wadau hao walitembelea miradi miwili ya hoteli zinazojengwa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika eneo ulipo mji wa Serikali Mtumba (Government City Complex) na Dodoma City Hotel inayojengwa katikati ya Jiji la Dodoma eneo la Paradise.
Ziara ya wadau hao katika miradi hiyo iliambatana na semina ya siku tano ya kubadilishana uzoefu kuhusu uendeshaji wa miradi mikubwa ya hoteli ambao mada mbalimbali ziliwasilishwa huku Halmashauri ya Jiji hilo ikitegemea kuingia kwenye biashara ya uendeshaji wa hoteli kwa kushirikiana na wadau mara baada ya miradi hiyo kukamilika hivi karibuni.
Sehemu ya Mradi wa kitenga uchumi cha Jiji (Government City Complex) unaoendelea kujengwa katika la Mtumba ulipo mji wa Serikali
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.