WADAU wa maendeleo hasa wanaoshughulikia masuala ya wanawake wameaswa kuelekeza rasilimali na afua zaidi katika kuwasaidia wanawake wanaoishi vijijini ambao ndio wazalishaji wakubwa wa malighafi za viwanda na mazao ya chakula katika Kaya na ndio wachangiaji wakuu wa pato la Taifa.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima ameyasema hayo alipozungumza na wananchi katika kata ya Mang'ula, Halmashauri ya mji wa Ifakara, wilaya ya Kilombero, mkoani Morogoro aliposhiriki maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mwanamke anayeishi kijijini, Oktoba 15, 2022.
Waziri Dkt. Gwajima amesema kuwa Wanawake hasa wa vijijini ndio wanapata changamoto nyingi zaidi kutokana na mgawanyo wa majukumu katika familia, uwezo mdogo wa kipato, elimu na ujuzi duni, mila na desturi kandamizi, ukubwa wa wategemezi katika Kaya na udhaifu wa miundombinu iliyopo Vijijini, hivyo ni muhimu sana kuimarisha ustawi na maendeleo yao ili kupunguza changamoto zinazowakabili.
"Serikali imeamua kuimarisha Ustawi na Maendeleo ya Mwanamke anayeishi kijijini ili kuleta mabadiliko endelevu yatakayonufaisha jamii kwa ujumla na kumpunguzia huyu mama anayeishi kijijini athari mbalimbali zinazotokana na mabadiliko ya Tabianchi ikiwa ni pamoja na Njaa, Ukame na Mafuriko yanayoweza kuleta madhara ya kuharibu Nyumba zilizo dhaifu". Amesema Mhe. Dkt. Gwajima.
Ameongeza kwamba Maadhimisho hayo yanatumika kuhamasisha Wadau kuelekeza Rasilimali kwa wanawake waishio vijijini ambapo matokeo yake ni yatawezesha kuainisha mbinu za kuamsha Ari ya Wadau kuboresha hali na mazingira ya vijijini kwa kutoa kipaumbele katika kushughulikia changamoto, mahitaji yao na kuunga mkono jitihada za Wanawake Waishio Vijijini na kuandaa Mifumo ya kukusanya Takwimu za mchango wa Wanawake Waishio Vijijini katika kuinua uchumi wa Taifa.
Aidha, Waziri Dkt Gwajima amesema majukumu hayo yatajenga uwezo wa Wanawake Waishio Vijijini kuthubutu kushiriki katika Siasa, Uongozi na nafasi za kutoa Maamuzi ili waweke msukumo katika kuelekeza Rasilimali, Nyenzo za Uzalishaji Mali na huduma za kifedha kwa Vikundi vya Wanawake na SACCOS zilizopo vijijini na kuelimisha jamii kuhusu Mila na Desturi kandamizi ili kuleta mgawanyo sahihi wa majukumu na Rasilimali katika familia na kupunguza mzigo wa kazi za Malezi, huduma kwa wanafamilia na kushiriki katika Uzalishaji mali kwa wanawake waishio vijijini.
Waziri Dkt. Gwajima amebainisha pia jitihada zinazofanywa Serikali katika kuwainua wanawake wanaoishi vijijini ni pamoja na kuwezesha marekebisho ya sheria ya mamlaka za Serikali za Mitaa inayotoa fursa kwa wanawake kupata asilimia 4 ya mkopo ya mapato ya ndani ya Halmashauri bil 28.1 ilitolewa kwa bikuni 4894 hadi mwaa 2021.
"Mkutano wa sita wa Baraza la uwezeshaji wannchi kiuchumi Taarifa zinasema kuwa kuna fursa zamikopo naprogramu 85 za uwezeshaji wananchi kiuchumi, kati ya hizo 75 ni za Serikali na 10 za binafsi ambapo kati ya hizo 24 ni za kumuwezesha mwananchi mmoja mmoja." alisema Waziri Dkt Gwajima
Mmoja wa Mkulima mwanamke Clara Male Mkulima amewashukuru wadau wanaoendelea kuwawezesha wanawake wa vijijini hasa wakulima na kutoa ushuhuda wake hadi sasa amefanikiwa kuunganishwa na masoko mbalimbali na kuweza kuuza mbegu za asili kwa wingi kupitia shirika la Pelum.
Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Sebastian Kitiku amesema Wizara inashirikiana na Wisara za Kisekta na Wadau wa maendeleo katika katika kuhakikisha wanawake hasa wanaoishi vijijini katika kuongeza nguvu za kuwawezesha Wanawake hao kujikwamua kiuchumi katika shughuli zao hasa Kilimo.
Naye Mwakilishi wa Chama Cha Mawakili Wanawake Tanzania (TAWLA) Sailasi Nyumba amesema kuwa lengo kuu la kuanzisha chama chao ni kutoa huduma za kisheria kwa wanawake hasa wanoishi vijijini ili waweze kusaidia kupunguza changamoto wanazokabiliana nazo katika shughuli zao za kiuchumi.
Maadhimisho ya Siku ya Mwanamke Anayeishi Kijijini yanaadhimishwa kwa mara ya tano nchini Tanzania, ambapo Lengo la maadhimisho haya ni kutambua mchango wa Mwanamke Anayeishi Kijijini katika Kilimo, uhakika wa chakula na kuinua uchumi wa Kaya na Taifa kwa ujumla.
Kaulimbiu ya maadhimisho haya kwa mwaka huu ni, "Mwanamke Aishiye Kijijini ni Mzalishaji Mkuu wa Chakula Tumuwezeshe".
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.