WADAU wa maendeleo ya vijana katika mkoa wa Dodoma wametakiwa kushirikiana katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya vijana ili kuwainua vijana kiuchumi na kuwa na afya bora ili kuwawezesha vijana kutimza ndoto zao maishani.
Hayo yalisemwa na Afisa Vijana wa Mkoa wa Dodoma Tumsifu Mwasamale tarehe 22 Januari, 2021 alipokuwa akifungua kikao cha pamoja cha wadau wa masuala ya uzazi kwa vijana katika jiji la Dodoma kwa mwaka 2021 kilichoandaliwa na Taasisi ya Maendeleo ya Vijana mkoani Dodoma (DOYODO) kwa lengo la kujadili changamoto ya mimba za utotoni na kuweka mikakati ya pamoja ya kupunguza mimba hizo.
Mwasamale akiongea katika ufunguzi huo aliwapongeza DOYODO kwa kuandaa kikao hicho muhimu cha wadau kwa mwaka 2021 na alitumia nafasi hiyo kuwaomba wadau wazidi kushirikiana katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya vijana jijini Dodoma.
Naye Mtendaji Mkuu wa DOYODO Rajabu Juma Suleiman aliahidi kuendelea kushirikiana na wadau katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya vijana hususani zinazolenga kumlinda mtoto wa kike.
Mratibu wa Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali Jijini Dodoma Mmsa Masuai Mmasa aliyakumbusha mashirikia kuendelea kufuata sheria na taratibu za NGO’s katika ufanyaji wa shughuli za kila siku.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.