MKUU wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Vijana wa Jiji la Dodoma, Sharifa Nabalang’anya amewasisitiza watumiaji wa vyombo vya moto wakati wa uzinduzi wa MILIKI CHOMBO NMB – Mastaboda, uliofanyika katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma wenye lengo la kuwawezesha vijana kupata mikopo ya bodaboda na bajaji.
Akizungumza katika uzinduzi huo alisema waipende kazi yao ili waimarike kiuchumi, wavae mavazi ya kupendeza pia wawe na lugha nzuri kwa wateja vilevile kuzingatia sheria za barabarani kwani abiria wengi wanapenda madereva wenye umakini.
“Sheria za barabarani ni muhimu kuzingatia na abiria wengi hupenda madereva wenye umakini, lakini pia ni muhimu kuwa na bima za afya, ajali zina epukika, lakini pale zinapotokea basi tupate ukombozi katika matibabu” alisema Nabalang’anya.
Nabalang’anya aliongeza kuwa ni vyema kuanza kufanya uokozi wa pesa kwa kujiwekea kwa ajili ya kukuza uchumi ambapo ni lazima kuachana na mambo yanayofanya matumizi ya pesa yawepo bila sababu ya msingi.
“Niwatoe hofu NMB kuhusu umoja huu, lakini nasisitiza maendeleo chanya katika marejesho na uaminifu hii ni njia moja wapo ya kuweza kuaminika na taasisi nyingine” alisema Nabalang’anya.
Mkutano huo ulioratibiwa na benki ya NMB kupitia Halmashauri ya Jiji la Dodoma ambapo tayari mkopo wa kununua bodaboda 46 na bajaji 21 umekwisha toka, na kila mwezi matarajio ya Shilingi Milioni 12.6 kama marejesho katika kuendeleza mradi huo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.