MKUU wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule, amefungua mafunzo ya siku moja kwa Maafisa biashara, Maafisa Maendeleo ya jamii na Maafisa TEHAMA juu ya usajili wa wafanyabiashara ndogondogo kwenye Mfumo wa utambuzi kwenye ukumbi wa ofisi yake iliyopo Jijini Dodoma.
Mafunzo hayo yanalenga kuchochea maendeleo ya wafanyabiashara ndogondogo nchini ambayo ni ajenda ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa wafanyabiashara watambuliwe na waunganishwe na mifumo ya fursa za kiuchumi.
“Jukumu lililopo mbele yetu baada ya mafunzo haya ni kwenda kufanikisha zoezi la utambuzi, usajili na wa vitambulisho kwa wafanyabiashara ndogondogo nchini hasa kwa Mkoa wetu wa Dodoma. Tunategemea juhudi zenu za kujituma katika kusimamia zoezi hilo kwa karibu pamoja na kushirikiana na Maafisa Mkoa ili kufikia lengo lililokusudiwa” Amesema Mhe. Senyamule.
Mkuu wa Mkoa huyo ameongeza kuwa, Mfumo wa utambuzi, usajili na utoaji wa vitambulisho kwa wafanyabiashara ndogondogo nchini, umekamilika baada ya kufanyiwa maboresho makubwa ili uweze kutoa vitambulisho vya kidijitali kwa wafanyabiashara ndogondogo kote nchini.
Aidha, Mfumo huo utasaidia katika kuwatambua wafanyabiashara ndogondogo na kuwasajili, kutoa vitambulisho vilivyounganishwa na Mfumo wa NIDA pamoja na kutoa vitambulisho vitakavyowawezesha wafanyabiashara ndogondogo kupata fursa zaidi za kiuchumi ikiwemo mikopo yenye masharti nafuu kutoka kwenye Taasisi za fedha.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.