Meneja wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira Kanda ya Kati Bwana Carlos Mbuta amekutana na viongozi pamoja na wafanya Biashara wa Soko la Majengo Jijini Dodoma ili kuwafikishia tamko lililotolewa na Baraza hilo kuhusu uwekwaji wa anuani kwenye vifungashio.
Akizungumza na wafanya biashara hao Mbuta amesema Baraza hilo limetoa siku 15 kwa wafanya biashara kuhakikisha wanamaliza kutumia vifungashio visivyokuwa na anuani ya muuzaji, na baada ya hapo faini itatozwa kwa mfanyabiashara yeyote atakaekiuka agizo hilo.
Nae mwenyekiti wa Soko hilo Bw. Hamis Bomu amesema agizo sio baya kwani anaamini Serikali kupitia Baraza hilo wana nia nzuri kwa maendeleo ya Jiji na Taifa isipokua ameomba waongezewe muda ili waweze kumaliza vifungashio ambavyo tayari walishavinunua.
Saidi Khamis ni mfanyabishara katika soko hilo yeye kwa upande wake amesema hatua hiyo yakuwataka tena watumie vifungashio vyenye anuani ya muuzaji inawachanganya wafanyabishara kwani walishatekeleza agizo la kuacha kutumia vifungashio vya plastiki na kununua kwa wingi vifungashio vilivyoelekezwa hapo awali.
Akihitimisha baada ya kusikiliza kero na mawazo kutoka kwa uongozi na wafanyabiashara sokoni hapo Mbuta amewataka wafanyabiashara hao waanze utekelezaji wa agizo hilo nayeye atafikisha malalamiko yao sehemu husika ili yafanyiwe kazi.
Mmoja wa wafanyabiashara wa Soko kuu la Majengo akichangia wakati wa mkutano na Meneja wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira Kanda ya Kati Bwana Carlos Mbuta na viongozi wa Soko Kuu la Majengo.
Meneja wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira Kanda ya Kati Bwana Carlos Mbuta akiongea na viongozi na wafanyabiashara wa Soko la Majengo kuwaeleza kuhusu utekelezaji wa kuweka anuani kwenye vifungashio.
Saidi Khamis ni mfanyabishara wa Soko Kuu la Majengo akichangia mada wakati wa mkutano na Meneja wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira Kanda ya Kati, mkutano uliofanyika sokoni Majengo.
Mwenyekiti wa Soko la Majengo Hamis Bomu ameridhia agizo la Serikali kupitia Baraza hilo lakini wameliomba baraza kuwapa muda zaidi kabla ya utekelezaji wa adhabu kwa watakaokiuka kuanza kutumika.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.