Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Majengo hapa jijini Dodoma wamekumbushwa kulifanya zoezi la usafi wa mazingira kuwa endelevu ili kuendelea kuboresha mazingira na afya zao na walaji wa bidhaa zao.
Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Idara ya Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu wa Jiji la Dodoma Dickson Kimaro baada ya shughuli za usafi kufanyika sokoni hapo kwa kushirikiana na wafanyabiashara wa soko la Majengo walipofanya zoezi la usafi wa mazingira katika maeneo yanayozunguka soko hilo leo.
Kimaro aliwakumbusha kuwa zoezi la usafi wa mazingira linatakiwa kuwa tabia kwa wakazi wa Jiji la Dodoma na ndio maana Mkuu wa Mkoa alitoa agizo kuwa zoezi hili litakuwa endelevu kwa kila mwananchi wa Jiji hili katika maeneo ya makazi na shughuli zao za kila siku.
Katika tangazo lake kwa wananchi wa Jiji la Dodoma, Mkurugenzi wa Jiji hilo amekuwa akikumbusha kwa taasisi, wafanyabiashara na wananchi wote kushiriki kutekeleza agizo la kufanya usafi wa kila Jumamosi umbali wa mita tano kuzunguka maeneo ya makazi na biashara ikiwa ni pamoja na kuwa na chombo cha kuhifadhi taka na kutojishughulisha na uchafuzi wa mazingira kwa njia ya sauti (kupiga kelele), utupaji wa takataka hovyo katika maeneo ya wazi, barabara, mitaro, mifereji na hata kufanya matengenezo ya vyombo vya moto kwenye maeneo yasiyo rasmi.
Naye Afisa Afya Usafishaji wa Jiji la Dodoma, John Lugengo amesema, mwitikio wa wafanyabiashara umekuwa mzuri, na akasisitiza kuwa wataendelea kushirikiana na wafanyabiashara wa masoko mengine pia ili kuweka mazingira rafiki kwa afya za wafanyabiashara wenyewe na walaji wa bidhaa za sokoni katika Jiji la Dodoma.
Tazama picha mbalimbali wafanyabiashara wa Soko la Majengo wakishiriki usafi wa maeneno yao ya biashara.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.