WAKAZI wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wametakiwa kutumia fursa ya chuo cha mafunzo ya ufugaji Nyuki kilichopo Mkoani Tabora ili kunufaika na elimu ya ufugaji Nyuki nchini.
Ushauri huo umetolewa na mmoja ya wakufunzi katika Chuo hicho, Mohamed Wawa alipokuwa akielezea fursa za chuo hicho kwa wakazi wa Jiji la Dodoma jana katika uwanja wa Nyerere square katika maadhimisho ya siku ya Nyuki duniani.
Wawa alisema kuwa chuo cha mafunzo ya ufugaji Nyuki- Tabora ni fursa kwa wakazi wa Jiji la Dodoma ambapo wanajishughulisha sana na kazi ya ufugaji Nyuki.
”Natoa wito kwa Wakazi wa Jiji la Dodoma, kutumia fursa ya chuo cha mafunzo ya ufugaji Nyuki –Tabora ili kupata elimu bora ya ufugaji Nyuki” alisema.
Alisema kuwa, katika kukidhi kiu ya Watanzania, chuo hicho kinatoa kozi kwa ngazi ya Stashahada na Cheti katika masomo ya ufugaji Nyuki na mazao yake.
“Chuo pia kinatoa mafunzo ya muda mfupi hadi wiki moja kwa utaratibu maalum kwa watu waliojiunga katika vikundi kwa lengo la kujifunza ufugaji Nyuki kisasa” aliongeza.
Maadhimisho ya siku ya Nyuki duniani mwaka 2019 yalifungwa na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda, yakiongozwa na kaulimbiu isemayo “Tuwalinde Nyuki kwa maendeleo yetu” ambapo yalishirikisha taasisi nane za Serikali na wajasiriamali 17 wa bidhaa za Nyuki.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.