• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Waganga Wafawidhi wa Jiji la Dodoma wapatiwa mafunzo ya Mfumo wa NeST

Imewekwa tarehe: January 29th, 2025

Na. Halima Majidi, DODOMA

Waganga wafawidhi kaitka Halmashauri ya Jiji la Dodoma wamewezeshwa mafunzo ya ununuzi kwa njia ya mfumo serikalini ‘National e- Procurement System of Tanzania’ (NeST) yatakayoongeza ufanisi na kurahisisha utendaji wa kazi pamoja na kupunguza hoja za ukaguzi kwa sababu kila kitu kitakuwa kipo wazi.

Mafunzo hayo yalitolewa na Kitengo cha Manunuzi na Ugavi cha Halmashauri ya Jiji la Dodoma, kwa lengo la kuongeza ufanisi, kupunguza gharama pamoja na kuokoa muda, ambayo yalifanyika katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Umonga.

Mwezeshaji wa Mafunzo hayo, Josephat Nyumayo, alieleza kuwa, mafunzo hayo yalikuwa yanahusu matumizi ya mfumo wa ‘NeST’ katika ngazi ya kata kwa mujibu wa Sheria ya Manunuzi ya Mwaka 2023 na Kanuni zake za Mwaka 2024, ikiwa ni utekelezaji wa agizo la serikali kuwa manunuzi yote yafanyike kwa mfumo huo.

Aidha, Nyumayo alisema kuwa, mafunzo hayo ni ya awamu ya pili kwa waganga wafawidhi ambapo mafunzo ya awali yalikuwa yanahusu matumizi sahihi ya mfumo wa ‘NeST’ na leo wameongeza kipengele cha uundaji wa kamati ambazo zimeleta mabadiliko kulingana na muongozo pamoja na sheria mpya. “Mwanzo kulikuwa na kamati tatu ambazo ni kamati ya ujenzi, manunuzi na mapokezi kwa mujibu wa sheria iliyofanyiwa marekebisho na muongozo uliotoka unahusisha kamati mbili, kamati tendaji na kamati ya mapokezi na majukumu ambayo yalikuwa yanafanywa na kamati ya manunuzi yatafanywa na Afisa Manunuzi alierasimishwa madaraka hayo” alisema Nyumayo.

Nae, Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Kikuyu, Azania Silliah, alisema kuwa anamshukuru Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kuwapatia mafunzo hayo, kwa sababu ameweza kutumia mfumo huo kwa kufanya manunuzi na kutoa tuzo kwa wale ambao wameomba ili waweze kupatiwa mahitaji.

“Kwahiyo, nawashauri waganga wafawidhi wenzangu na watu wengine, haya mafunzo ni mazuri, tusiyaogope kwanza ni ya uwazi pia yanaepusha hoja za ukaguzi maana kila kitu kipo wazi” alishauri Silliah.

Kwa upande wake, Mtumishi wa Zahanati ya Chololo, Samwel Karidushi, alisema kuwa, mafunzo ameyapokea vizuri, ataenda kuwaelekeza na kuwa mwalimu kwa watumishi wenzake ili kurahisisha uagizaji wa vifaa. “Mfumo huu unalenga kusaidia kupunguza gharama ikiwemo nauli za uagizaji wa vifaa pamoja na ufuatiliaji wa taarifa mbalimbali katika taasisi” alisema Karidushi.

Vilevile, Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Chididimo, Isaka Witiche, alisema kuwa, anamshukuru Mkurugenzi kwa Jiji la Dodoma, kwa kushirikiana na Ofisi ya Mganga Mkuu wa Jiji la Dodoma, kwa kuwapatia mafunzo ya manunuzi kwa njia ya kidigitali na kuahidi kwenda kuyatekeleza. “Kama tulivyoelekezwa kununua vifaa kwa njia ya kidigitali tutaenda kuhakikisha tunaleta mabadiliko katika vituo vyetu vya kazi” alisema Witiche.




Matangazo

  • TANGAZO LA MABADILIKO YA TAREHE YA USAHILI October 03, 2025
  • TANGAZO LA MAJINA YA WASIMAMIZI JIMBO LA MTUMBA October 03, 2025
  • MAJINA YA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA- DODOMA MJINI October 03, 2025
  • TANGAZO LA MAJINA YA MAKARANI WAOGOZAJI WAPIGA KURA October 03, 2025
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Rc Senyamule awasihi wawekezaji sekta binafsi kuwekeza Dodoma

    October 03, 2025
  • CCTV kamera mwarobaini wa wavunjifu wa sheria jiji la Dodoma

    October 02, 2025
  • Wadau wa afya wapongezwa kwa juhudi zakudhibiti vifo vya wajawazito

    October 01, 2025
  • UONGOZI WA KLABU YA MICHEZO OFISI YA MKUU WA MKOA WA DODOMA WAKUTANA NA RAS KAZUNGU

    September 29, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.