WAHARIRI wa vyombo mbalimbali vya habari wametembelea mradi mkubwa wa kimkakati wa bwawa la kufua umeme wa maji la Julius Nyerere Hydro Power Project (JNHPP-2115) lililoko bonde la mto Rufiji na kujionea ujenzi ukiendelea kwa kasi usiku na mchana katika maeneo yote muhimu matano.
Wahariri hao wametembeela eneo la ujenzi wa bwawa (Main Dam), eneo la kuchepusha maji (Diversion Tunnel), eneo la (Power Intake) na eneo la kufua umeme (Power Generation).
Lakini pia wahariri hao wametembelea maeneo mengine ya ujenzi kama vile eneo la kuchukulia umeme (Switch Yard) na sehemu ya mitambo ya kuchanganya zege.
Wahariri wa wameonyesha kufurahishwa na ziara hiyo ambapo kwa nyakati tofauti wamepongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa uamuzi wake wa kutekeleza mradi huo kwa gharama za watanzania wenyewe kwa sababu hii ilikuwa ndoto ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Akielezea utekelezaji wa mradi huo Kaimu Mhandisi Mkazi wa ujenzi wa Bwawa la Julius Nyerere Hydro Power Project (JNHPP) Lutenganya Kamugenyi amesema ujenzi wa mradi huo unaendelea usiku na mchana ambapo pia tahadhari zote zinazoweza kukwamisha shughuli za ujenzi zimechukuliwa hata mvua ikinyesha ujenzi utaendelea kama kawaida.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.