Na. Mwandishi wetu, DODOMA
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri ametoa rai kwa wahitimu wa Chuo cha Kati cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Dodoma (DOMECO) kuwa waandishi mahili kwa kufanya utafiti.
Shekimweri alitoa hiyo katika mahafali ya Saba ya Chuo hicho kwa wahitimu wa ngazi ya Astashahada na Stashahada ya Uandishi wa Habari na Utangazaji akiwataka kuyaishi maadili ya Uandishi wa Habari kwa sababu ni chachu ya mabadiliko katika Taifa.
Alisema kuwa wahitimu hao wanawajibu wa kufuata watu sahihi wa kuwapa taarifa kamili ambazo hazina udanganyifu na kufanya uwiano wa taarifa za pande zote mbili na aliwahamasisha wanafunzi kutafuta vyanzo mbalimbali vya habari na kujifunza jinsi ya kuchambua taarifa.
“Ujuzi na ubunifu wa kuandika kila mtu ananamna yake ya kuandika na kila mtu Mungu kampatika karama. Karama mlizopatiwa mzitumie vizuri, hebu tuone upekee wa mwandishi huyu na mwandishi mwingine, niwatie shime pia muwe na uelewa wa maudhui, muwe wajasili. Mwisho kabisa muwe na mawasiliano mazuri na watu wa kuwapatia taarifa sahihi” alisisitiza Shekimweri.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.