Wakazi wa Jiji la Dodoma wamekumbushwa kutekeleza wajibu wao wa kufanya usafi ili kulifanya Jiji la Dodoma kuwa safi na la kuvutia muda wote.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Idara ya Mazingira na Usafi wa Taka ngumu wa Jiji la Dodoma, Dickson Kimaro alipokuwa akiongea na wananchi waliojitokeza kufanya usafi siku ya Jumamosi katika Kata ya Kiwanja cha Ndege jijini hapa.
Aidha alitoa wito kwa Watendaji wa Kata na Mitaa kuhakikisha wanasimamia maelekezo hayo kikamilifu ili wananchi wajitokeze kwa wingi kufanya usafi katika makazi na biashara zao mita tano kuzunguka maeneo yao na kujiepusha na utupaji holela wa taka kwenye maeneo yasiyoruhusiwa.
"Usafi wa mazingira yetu utatuwezesha kuwa salama kiafya na kupunguza uwezekano wa kutokea magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu, kuhara na kadharika" alisistiza Kimaro.
Vilevile, Kimaro amewahimiza wakazi wa Jiji la Dodoma kupanda miti ya matunda na ile yenye kuleta kivuli katika msimu huu wa mvua. “Faida ya miti sote tunaifahamu, miti hutusaidia kupata matunda na kivuli kwa ajili ya mapumziko, lakini pia tukipanda miti itasaidia kupunguza hali ya joto hasa wakati wa kiangazi, pia hupunguza kasi ya upepo uvumao na kwamba miti huongeza thamani ya maeneo tunayoishi.
Tazama picha na matukio wakati wa usafi kata ya Kiwanja cha Ndege Jumamosi Novemba 5, 2020.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.