Na Noelina Kimolo.
“WAGONJWA wa COVID-19 wapo hivyo wakazi wa Dodoma wasichukulie mzaha suala hili wajitahidi kuchukua tahadhari za kujikinga kama vile kunawa mikono kwa maji tiririka, kutumia vitakasa mikono pamoja na kuepuka misongamano isiyo ya lazima ili kuepuka maambukizi”.
Kauli hii imetolewa na mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Gasper Kisenga wakati akifanya mahojiano katika kipindi cha Tuongee Asubuhi kinachoruswa na kituo cha Star Televisheni cha jijini Mwanza.
Dkt. Kisenga alisema kuwa, katika kupiga vita ugonjwa wa COVID-19 wameweza kuzungumza na wadau mbalimbali kama vile wadau wa elimu, jeshi la porisi, wenyeviti wa masoko pamoja na viongozi wote waliopo kwenye vituo vya mabasi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
“Wagonjwa wapo na ndio maana tunatoa elimu kwa wananchi na elimu hiyo iwafikie ili waweze kubadilika, na kufuata taratibu zote za kujikinga na ugonjwa wa COVID-19 huku wakiendelea na majukumu ya kila siku” alisema Dkt. Kisenga.
Alisema kuwa walikuwa na wadau wa elimu ambao anaamini hao watawasaidia kutoa elimu juu ya ugonjwa huo kwa wanafunzi wa shule za msingi sekondari pamoja na vyuo, huku wadau kutoka jeshi la polisi wakisaidia katika kupunguza msongamano ndani ya daladala, pia usafirishaji na wenyeviti wa masoko mbalimbali na stendi lengo likiwa kila mmoja atoe elimu kwenye eneo lake.
Dkt. Kisenga alisema kuwa, jukumu la kupambana na ugonjwa huo halipo kwa mtu binafsi bali ni kwa kila mtu mwenye ufahamu aweze kupambana nalo kuanzia nyumbani, barabarani, maeneo ya kazini na sehemu zote lazima tuchukue tahadhari za kujikinga na ugonjwa wa COVID-19.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.