Na. Coletha Charles, DODOMA
WAKAZI wa Mtaa wa Nala, Segue Juu, Segu Chini na Chihoni, wamewezeshwa elimu kupinga Ukatili wa kijinsia, Malezi na Makuzi, Uchumi na Afya ya uzazi katika Kata ya Nala Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Akizungumza wakati wa kutoa elimu ya Malezi na Makuzi, Afisa maendeleo ya Jamii Kata ya Chamwino, Cecilia Oswago, ambaye alimuwakilisha Mratibu wa Dawati la Jinsia Idara ya Maendeleo ya Jamii Fatuma Kitojo.
Alisema kuwa wazazi wanatakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuwalea watoto wao kwa kutenga muda wa kuzungumza nao na kuwajengea uwezo wa kuzungumza kipindi wakipata matatizo kwa kuzingatia haki ya mtoto na wajibu.
“Mnawaacha sana watoto wanajilea wenyewe, mama unapambana kwa ajili ya watoto unashinda kwenye mihangaiko unatoka asubuhi mtoto amelala unarudi unakuta kalala hujui mtoto kashindaje wala anashida gani. Lakini pia kuna mazoea tumejijengea wazazi na walezi kwenye vitu vya msingi vya watoto hatuvizingatii, tukumbuke tunawaumiza watoto kwa kuhisi kila kitu cha kawaida” alisema Oswago
Naye, Afisa Maendeleo Kata ya Nala, Monica Lugaila, aliwezesha elimu ya ukati na afya uzazi na kuwataka wazazi kuwa mstari wa mbele kupinga ukatili kwa watoto kwa kutowaozesha wakiwa na umri mdogo.
“Mnawaozesha watoto wadogo mno, akijifungua unakuta anapata changamoto kibao hadi unamuonea huruma. Lakini pia wazazi msifumbie macho watoto wanapofanyiwa ukatili nendeni mkashitaki mahali husika mpate msaada wa haraka” alisema Lugaila.Aidha, Afisa Mradi wa Ahadi Shirika la Tahea, Zaituni Liendekiye, alitoa elimu ya uchumi kwa vijana kuchangamukia fursa zinazotolewa na shirika hilo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.