Na. Hellen M. Minja,
Habari – DODOMA RS
Takribani wakulima 40,000 wa zao la Mtama Mkoa wa Dodoma, wanatarajiwa kunufaika na kilimo hicho kutokana na utekelezaji unaoendelea wa Mradi wa ‘Climate Smart Agriculture Project (CSAP)’ ambao ni wa miaka minne (2022-2026) kwa ufadhili wa Irish Aid chini ya Shirika la Chakula Ulimwenguni WFP.
Hayo yamebainishwa na Balozi wa Ireland Nchini Tanzania Bi. Nicola Brennan, alipomtembelea Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ofisini kwake Jengo la Mkapa Jijini Dodoma kumfahamisha maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo.
Lengo la mradi ni kupambana na mabadiliko ya tabia nchi,umewekeza zaidi kwenye zao la mtama kutokana na sifa yake ya kuhimili mabadiliko hayo, huku ukilenga zaidi kuwainua wakulima wanawake kiuchumi kwani soko lake linafikia shilingi Bilioni 3.08
Mhe. Senyamule amefurahishwa na utekelezaji wa Mradi huo na ameishuku Serikali ya Ireland kwa ufadhili kwani moja ya vipaumbele vya Mkoa wa Dodoma mwaka huu ni kuinua uchumi wa Wanadodoma, ikizingatiwa kuwa 72% ya wakazi wake ni wakulima hivyo, Mradi huo utasaidia kufikia malengo ya Mkoa kwa haraka.
Vijiji 222 vinavyopatikana katika Wilaya sita (6) za Mkoa wa Dodoma vinatarajiwa kufikiwa na Mradi hadi kufikia 2026 ambapo Mradi utakua umemaliza muda wake. Balozi huyo atatembelea mradi unaotekelezwa kwenye Halmashauri za Chamwino na Bahi.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.