AFISA Kilimo katika halmashauri ya Jiji la Dodoma Athumani Mpanda amesema wakulima wa wilaya ya Dodoma watapata mbegu za kutosha za zao la alizeti zinazouzwa Halmashauri hiyo kwa ajili ya msimu mpya wa kilimo cha zao hilo unaotarajiwa kuanza mwezi Disemba 2021.
Mpanda alisema hayo wakati alipotembelea ghala la mbegu la Halmashauri hiyo kwa ajili ya kuanza utaratibu wa kusafirisha mbegu hizo katika kata mbalimbali za Jiji hilo ambapo alisema viongozi wa ngazi ya kata ndiyo wenye jukumu la kuuza mbegu hizo kwa wakulima katika husika.
Afisa Kilimo huyo alisema bei ya mbegu hizo ni ruzuku ambapo kilo moja inauzwa shilingi 3,500 badala ya shilingi 10,000 baada ya serikali kulipia sehemu ya gharama ili wakulime waweze kumudu na kuhamasika kulima zao hilo la kimkakati kwa lengo la kufuta kabisa changamoto ya upungufu wa mafuta ya kula nchini.
Alitoa wito kwa wakulima katika mikoa mitatu ya Dodoma, Singida na Simiyu ambako ndiko serikali imelipa ruzuku ya mbegu hizo kulima zao hilo ili kutumia fursa hiyo kujiinua kiuchumi.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.