Wadau wa Uuguzi na Ukunga wamekutana na kupanga mikakati ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga kwa kuhakikisha huduma zinakuwa bora ikiwa ni pamoja na kushirikisha walimu wa vyuo mbalimbali vinvyozalisha wanafunzi wa taaluma hiyo.
Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa huduma na Ukunga na Uuguzi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Ziada Sellah wakati akifungua semina fupi kwa niaba ya Mganga mkuu wa Serikali ambapo semina hiyo iliwashirikisha Wizara ya Afya, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, wakufunzi wa vyuo na Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA) kwenye hospitali ya Benjamin Mkapa jijini hapa.
"Tumeangalia kwa upana wake na kuweka mikakati mbalimbali ya jinsi huduma zinazotolewa na wakunga kwa wajawazito ikiwa ni pamoja na kuwapa mazingira wezeshi, huduma nzuri kwa wateja lakini pia tumewashirikisha walimu wa vyuo vya ukunga ili wafundishe somo la huduma kwa mteja ili isijekuwa ni kitu kipya kwa wanafunzi wanapoingia kazini" amesema Bi. Ziada.
Bi. Ziada amesema Wizara kupitia kurugenzi ya Uuguzi na Ukunga itahakikisha wakunga wanapata mafunzo wakiwa maeneo yao ya kazi kupitia kwa wauguzi wakuu wa Wilaya na Mikoa pamoja na wauguzi viongozi ili kuweza kuboresha ukunga lengo ikiwa ni kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.
"Tumeangalia kwa upana kuanzia huduma zinapaoanza kutolewa upande wa huduma ya Uzazi, Mama na Mtoto pale mama anapoanza kliniki na kuelekeza jinsi gani ya kutoa huduma ikiwemo vidokezo hatarishi kwa mama mjamzito pamoja na kutoa rufaa mapema endapo kesi hawatoiweza, hivyo tutawajengea uwezo wakunga kwani asilimia 90 ya akina mama wote wanaojifungua wanahudumiwa na wakunga" alisisitiza Bi. Ziada.
Naye rais wa Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA) Bi. Fedy Mwanga amesema chama kimejidhatiti kutoa elimu kwa wauguzi na wakunga nchini kuhusiana na huduma bora za uzazi kwa mama mjamzito kabla na baada ya kujifungua lengo likiwa ni kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.
Washiriki wa semina katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa huduma na Ukunga na Uuguzi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Ziada Sellah (wa pili kushoto waliokaa)
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.