KATIBU MKUU wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa (Tamisemi), Prof. Riziki Shemdoe amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri 22 ambao hawajaingiza taarifa zao za hesabu za mwisho kwenye mfumo wa Serikali wa uandaaji wa hesabu kufanya hivyo ndani ya siku mbili.
Prof. Shemdoe amesema ifikapo Septemba 30, 2021 ambao watakuwa bado hawajatekeleza agizo hilo wajiandae kwa kupata hati chafu au zenye mashaka.
Amezitaja baadhi ya Halmashauri hizo kuwa ni Jiji la Dar es Salaam (Jiji la zamani), Mvomero DC, Chalinze DC, Madaba DC, Shinyanga DC, Muheza DC, Kishapu DC, Kahama MC, Lushoto DC, Bahi DC, Newala DC, Newala TC, Kibaha DC, Songea DC, Itilima DC, Manyoni DC, Songwe DC, Bumbuli DC, Kilindi DC na Msalala DC.
Katibu Mkuu huyo wa TAMISEMI ameyasema hayo leo tarehe 24 Septemba 2021 Jijini Dodoma wakati wa mafunzo ya siku mbili ya Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.