NAIBU Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga ametoa wito kwa Wakurugenzi wa Halmashauri kutenga bajeti kwa ajili ya kuwawezesha Maafisa wanaosimamia Elimu ya Watu Wazima kuwafikia walengwa kwa urahisi.
Kipanga ametoa wito huo wakati akifunga maadhimisho ya Juma la Elimu ya Watu Wazima yaliyofanyika katika Viwanja vya DUCE Jijini Dar es Salaam ambapo amesema kwa kufanya hivyo itawezesha utekelezaji wa shughuli za elimu ya watu wazima katika eneo husika kwa ufanisi.
Amesema katika kuipa uhai elimu ya watu wazima pamoja na kutengewa bajeti maafisa elimu wanaoshughulika na eneo hilo ndani ya Mikoa na Halmashauri wanapaswa kuhakikisha wanahamasisha, kuanzisha, kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa Programu mbalimbali za Elimu ya Watu Wazima.
"Niwasihi Maafisa Elimu Elimu ya Watu Wazima pamoja na kusimamia kazi katika maeneo yenu shirikianeni na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima kuendeleza jitihada za kuhakikisha kuwa madarasa ya MEMKWA yanasimamiwa na kuwa na vitendea kazi vinavyokidhi mahitaji ya ufundishaji na ujifunzaji," amesema Kipanga.
Akizungumzia mapitio ya Sera na mitaala yanayoendelea Kipanga amesema Wizara bado inapokea maoni ya wadau kuhusu maboresho hayo huku ikiendelea na uchambuzi wa maoni ambayo yamepokelewa ili kukamilisha kazi hiyo.
Amesema kumekuwa na taarifa ambazo si za kweli zinazosambaa kwenye mitandao zikisema kuwa "Sera ya Elimu inayotarajiwa kuzinduliwa hapo baadae elimu ya msingi itakomea darasa la sita."
"Nilikuwa kwenye Kongamano la Wanataaluma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wakati nazungumza nilisema kuwa tunaendelea na mapitio ya Sera ya Elimu na kwamba kuna maoni mbalimbali yameshatolewa na katika uchambuzi yapo maoni yaliyosema elimu ya msingi ikomee darasa la sita na baada kumaliza kuwe na mifumo na njia mbili kuu ambazo zinawapeleka vijana kwenye taaluma na ujuzi. Sasa zipo nukuu kwenye mitandao zikisema nimesema elimu ya msingi mwisho5 darasa la sita si kweli", amefafanua Kipanga.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.