• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

"Wakurugenzi msiingie mtegoni" - Waziri Jafo

Imewekwa tarehe: October 3rd, 2019

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Seleman Jafo amewatahadharisha wakurugenzi wapya walioteuliwa hivi karibuni kukwepa mtego uliowanasa wenzao walioondolewa madarakani na badala yake wakajenge mshikamano na umoja kwa watumishi watakao wakuta kwenye vituo vyao vipya vya kazi.

Akizungumza katika kikaokazi na Wakurugenzi hao kilichokwenda sambamba na zoezi la kula kiapo cha Maadili kwa viongozi wa umma, Jafo amewatahadharisha viongozi hao dhidi ya baadhi ya watumishi watakao wapelekea majungu kwakujipendekeza na kutaka kuchonganisha watendaji na kuvuruga utendaji wa Halmashauri.

“Ajenda kuu ya Serikali hivi sasa ni ukusanyaji wa mapato, lakini pia usimamizi wa Miradi ya maendeleo ikiwepo fedha za vituo vya afya ambazo baadhi walishindwa kuzisimamia hivyo ili muweze kufanikiwa katika hili lazima mkatengeneze mahusiano   na morali miongoni mwa watumishi ili   msikwame na watu wachape kazi kwa hamasa kubwa” alisema Waziri Jafo.

Awali akitoa maneno ya utangulizi, Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mathias Kabunduguru, aliwataka wakurugenzi hao watambue huu ni mwaka wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa hivyo wakasimamie ipasavyo zoezi la kuandikisha wapiga kura litakalo anza tarehe 08 Oktoba, 2019.

“Idadi kubwa mlioteuliwa mlikuwa watumishi katika ngazi ya mamlaka ya Serikali za Mitaa, hivyo haitakuwa kazi sana, lakini yapo yale ambayo yalikuwa yanakukera ukiwa kama Afisa Tarafa unapoagizwa na Mkurugenzi, sasa hayo usiende kuwafanyia waliochini yako bali mkafanye kazi kwa ushirikiano” Alisema Kabunduguru.

Bw. Mohamed Mavura ni miongoni mwa Wakurugenzi wapya aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti mkoani Pwani, amesema kuwa anakwenda Kibiti akiwa anajua kabisa ipo Miradi ya Maendeleo, suala la mapato, lakini pia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu wa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 hivyo ameahidi kufanya kazi kwa umoja na mshikamano kama Waziri alivyowaasa.

Wakurugenzi waliokula kiapo hicho mbele ya Afisa Mfawidhi wa Sekretarieti ya Maadili ni pamoja na Bw. Ndaki Stephano Muhuli, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro, Bi. Rehema Said Bwasi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Bi. Sheillah Edward Lukuba, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro mkoani Morogoro, Bw. Mohamed Mavura Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti mkoani Pwani.

Wengine ni  Bw. Ezekiel Henrick Magehema, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya, Bi. Diana Sono Zacharia, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Butiama mkoani Mara, Bi. Hanji Godigodi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, Bw. Said H. Magaro Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui mkoani Tabora, Bi. Hawa Lumuli Mposi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Mkoani Morogoro, na Bw. Godwin Justin Chacha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro.



Matangazo

  • TANGAZO LA MABADILIKO YA TAREHE YA USAHILI October 03, 2025
  • TANGAZO LA MAJINA YA WASIMAMIZI JIMBO LA MTUMBA October 03, 2025
  • MAJINA YA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA- DODOMA MJINI October 03, 2025
  • TANGAZO LA MAJINA YA MAKARANI WAOGOZAJI WAPIGA KURA October 03, 2025
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Rc Senyamule awasihi wawekezaji sekta binafsi kuwekeza Dodoma

    October 03, 2025
  • CCTV kamera mwarobaini wa wavunjifu wa sheria jiji la Dodoma

    October 02, 2025
  • Wadau wa afya wapongezwa kwa juhudi zakudhibiti vifo vya wajawazito

    October 01, 2025
  • UONGOZI WA KLABU YA MICHEZO OFISI YA MKUU WA MKOA WA DODOMA WAKUTANA NA RAS KAZUNGU

    September 29, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.