Na Angela Msimbira, NZEGA
NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Zainab Katimba amewaelekeza wakurugenzi wa halmashauri nchini kuzingatia utengaji wa bejeti kupitia mapato ya ndani ili kuendeleza miundombinu ya sekta ya elimu.
Mhe.Katimba ametoa melekezo hayo alopokuwa akihitimisha ziara yake ya kikazi katika Mkoa wa Tabora kwenye eneo la ekari 23 litakalotumika kujenga shule ya amali katika Halmashauri ya Mji Nzega.
Amesema mamlaka za serikali za mitaa zina wajibu wa kuhakikisha zinaendeleza miundombinu ya elimu na kutoacha jukumu hilo kwa serikali kuu pekee.
“Pamoja na jitihada kubwa zinazofanywa na Mheshimiwa Rais Samia kuleta fedha nyingi za kutekeleza miradi katika sekta ya elimu ili kuhakikisha wanafunzi wetu wanapata elimu iliyobora, sasa mamlaka za seriali za mitaa zisiache jukumu la kuendeleza miundombinu iliyofanywa na Serikali kuu pekee bali jukumu la msingi ni la mamlaka za serikali za mitaa.”
Akizungumzia ziara hiyo, Mhe.Katimba amesema ametembelea maeneo tofauti tofauti na kukagua majengo katika shule mbalimbali ikiwemo shule ya sekondari ya sayansi ya wasichana ambayo Rais Samia Suluhu Hassan amepeleka Sh bilioni 4.1 na tayari imeshaanza kuchukua wanafunzi.
“Katika ukaguzi wa miradi hii katika sekta ya elimu tumepita na tumetizama miundombinu imara tumeshuhudia jitihada kubwa iliyofanywa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye anashusha fedha nyingi sana kwa ajili ya kuboresha miundombinu katika sekta ya elimu.”
Amesema kutokana na juhudi hizo za Rais Samia, watanzania wanapaswa kujua kuwa wanajukumu la msingi la kuendelea kuchangia katika kustawisha mazingira mazuri zaidi ya wanafunzi kupata elimu.
Pia amendeleea kusisitiza wasimamizi wa miradi ya ujenzi wa shule kuhakikisha wanafuata miongozo inayotolewa chini ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI.
Aidha, Mhe.Katimba amewahimiza wakuu wa shule kuhakikisha wanapanda miti ya matunda na kuandaa bustani za mbonga katika maeneo ya shule hatua ambayo itawafanya wanafunzi kupata lishe bora.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.